Monday, June 16, 2014
UFARANSA YAFAIDI TEKNOLOJIA YA GOAL.
Do you like this story?
Ufaransa
ndiyo timu ya kwanza kuwahi kufaidi matumizi ya teknolojia ya kisasa kuzuia
ubishi katika mechi ya kombe la dunia linaloendelea huko Brazil.
Karim
Benzema alikuwa anatekeleza mashambulizi katika lango la Honduras kunaklo
dakika ya 48 ya kipindi cha pili lakini kipa wa Honduras Noel Valladares
akababaika na mpira ukavuka laini kisha akaunyofoa mara moja na
kukimbia
akitaka kuupiga kama 'goal kick' lakini mpiga kipenga kutoka Brazil Sandro
Meira Ricci akapuliza kipenga na kuashiria bao kutokana na mtikiso kwenye saa
yake inayoambatana na teknolojia hiyo ya kisasa ya goal line.
Mashabiki
na wachezaji wa Honduras waliokuwa ndani ya uwanja wa Porto Alegre walijaribu
kupinga kauli ya refarii huyo lakini wapi alihakiki bao hilo la pili usiku huu
kwa Ufaransa .
Honduras
ilikuwa tayari imempoteza mchezaji wao Palacios mwisho wa kipindi cha kwanza
alipoonyeshwa kadi ya pili ya manjano
Teknolojia
hiyo inayotumika kwa mara ya kwanza inajumuisha kamera 14 za kisasa na zenye
uwezo mkubwa wa kurekodi picha na sauti kwa kasi mno na mpira ambao inasambaza
Kamera
hizo zinauwezo wa kuchukua picha kwa kasi mno (saba kwenye kila lango), katika
paa za nyanja zote 12, Brazili.
Kamera
hizi zimeunganishwa kwenye tarakilishi inayounda maumbo na kuondoa umbo lolote
lile ambalo sio la mpira, kisha kufuata mwenendo wa mpira kwa kadri milimita
chache, kampuni hiyo ilisema.
Mpira
unapovuka tu mstari wa lango, utakuwa unapeperusha ujumbe kwenye saa yake
mwamuzi wa mechi, kisha ujumbe wenye maandishi ‘GOAL’ unatokea kwenye saa hiyo
pamoja na mtikisiko (Vibration).
Haya
yote yanafanyika kwa muda wa chini ya sekunde moja.
Mfumo
huo ambao tayari ushajaribiwa na Fifa, katika kombe la Mashirika mwaka
uliopita.
Kampuni
ya Sony, ambayo inathamini mpango huo wa kiteknolojia wa Fifa, wameweka zaidi
ya kamera 224, zenye uwezo mkubwa, ambazo zitaonyesha zaidi ya saa 2500 ya
michezo.
Hii
itakua mara ya kwanza michuano ya kombe la dunia kuonyeshwa katika mfumo wa
kisasa wa kiteknolojia wa Ultra-High Definition (UHD), ujulikanao kama 4K
Format, ambayo kiwango chake ni mara nne zaidi ya kiwango cha
televisheni
za kawaida.
Hata
ingawa suluhisho hii imetumiwa kwa miaka mingi katika michezo mingine,kama
Tennis Cricketi na Raga hii itakua mara ya kwanza teknolojia ya lango la goli
kutumika katika kombe la dunia .
Ni
mfano mmoja tu wa jinsi kombe hili la dunia litakavyokua lenye teknolojia kubwa
zaidi na lenye kujumuisha miundo mbinu ya teknolojia ya karne ya 21.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “UFARANSA YAFAIDI TEKNOLOJIA YA GOAL.”
Post a Comment