Tuesday, June 10, 2014
WANAWAKE 20 WANAUME 3 WATEKWA NIGERIA
Do you like this story?
Wapiganaji
wanaoshukiwa kuwa wanachama wa Boko Haram wamewateka nyara wanawake 20 kutoka
jamii inayohamahama Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.
Wanawake
hao walichukuliwa katika Makazi ya Gakini Fulani karibu na mji wa Chibok ambako
zaidi ya wasichana wanafunzi 200 walitekwa nyara Aprili, mwaka huu.
Walioshuhudia
tukio hilo walisema kuwa wapiganaji hao waliokuwa wamejihami kwa bunduki
waliwalazimisha wanawake hao kuingia katika magari yao kabla ya kutoroka nao
katika Jimbo la Borno.
Mlinzi
mmoja wa kijiji alisema kuwa washambulizi hao pia waliwateka nyara wanaume
watatu waliojaribu kuwazuia wasiondoke na wanawake hao.
Hadi
sasa jeshi halijasema lo lote kuhusiana na tukio hilo.
Shambulio
hilo lilitokea katika mji wa Chibok ambako wapiganaji wengine wa silaha
waliwteka nyara zaidi ya wasichana 200 wanafunzi Aprili, mwaka huu.
Wakati
huo jeshi la Nigeria limesema kuwa limewaua wapiganaji 50 katika kampeni yake
dhidi ya magaidi mwishoni mwa wiki katika majimbo la Borno na Aladawa.
Mfululizo
wa mashambulizi Kaskazini Mashariki mwa taifa hilo umeimarisha ukosoaji wa
vyombo vya usalama vya Serikali.
Licha
ya kuwepo kwa hali ya hatari katika eneo la Kaskazini Mashariki mwa Nigeria
wanajeshi hawajachukua hatua dhabiti na wakati mwingine hawapo wakati
washambulizi wanaotekeleza uhalifu wao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “WANAWAKE 20 WANAUME 3 WATEKWA NIGERIA”
Post a Comment