Tuesday, June 10, 2014

CHUI WAZUA MTAFARUKU BAADA YA KUVAMIA KIJIJI MOSHI VIJIJINI.



WAKAZI wa kijiji cha Okeseni Chini,  Wilaya ya Moshi Vijijini, mkoani Kilimanjaro, wanalala mapema wakihofia kushambuliwa na kundi la wanyama aina ya Chui lililovamia kijiji hicho.

Akizungumza  kwa njia ya simu jana, mmoja wa wakazi hao, Pamfill Shayo, alisema hivi sasa wanakijiji hao wanaingia ndani saa 12 jioni na kulala wakiogopa kushambuliwa na chui hao ambao tayari wameshaua mifugo ipatayo 25.

Alisema kundi hilo la Chui limekuwa likirandaranda katika vichaka vilivyoko karibu na kijiji hicho na  kila giza linapoingia wanajitokeza, hali inayotishia usalama wa maisha yao.

“Hawa Chui hadi sasa wameua mbuzi, mbwa, paka na kuku. Hali inatisha uanajua mnyama huyu alivyo na vurugu wakati mwingine wanavamia kundi la mifugo na kuiua,”alisema Shayo.

Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Melkadeke Mushi, alikiri kijiji hicho kuvamiwa na wanyama hao.

Hata hivyo, alisema taarifa zimefikishwa kwenye Idara ya Wanyamapori, hivi sasa wanasubiriwa ili kuwarudisha katika maeneo ya hifadhi ya taifa.

0 Responses to “CHUI WAZUA MTAFARUKU BAADA YA KUVAMIA KIJIJI MOSHI VIJIJINI.”

Post a Comment

More to Read