Friday, July 4, 2014

JANUARY AJITOSA URAIS 2015



Naibu waziri wa mawasiliano sayansi na teknolojia, January makamba ametangaza nia yake ya kuwania urais akisema  huu ni wakati wa kupitsha fikra mpya kuongoza dola licha ya chama hicho kuzuia  kutangaza nia ya kupiga kampeni kabla ya muda.

Makamba mmoja wa makada wa CCM walioonywa  na chama hicho baada ya kutuhumiwa  kuanza kampeni mapema alijipigia  debe kuwa  iwapo atapitishwa na chama hicho ataelekeza  nguvu kwenye  vipaumbele  vyake vine ambayo ni ajira huduma za jamii uchumi imara na utawala bora.

Mbunge huyo wa bumbuli alisema hayo akiwa uingereza anakohudhuria mkutano wa sekta ya mawasiliano baada ya kuhojiwa na shirika  la utangazaji la uingereza na baadaye  kufafanua nia hiyo  katika  mahojiano na mwananchi jana.

Mwandishi huyo wa zamani wa hotuba za rais jakaya kikwete alisema  hadi sasa ameshafanya  uamuzi wa asilimia 90  kujitokeza kuwania nafasi hiyo ya juu kuliko zote nchini bado asilimia 10  katika baadahi ya mambo ambyo anaendelea  kuyatafakari  kuzungumza na makundi mbalimbali ya wazee viiongozi  wa dini na viongozi waliopita ili nipate ushauri wao kuhusu namna ya kufanya jambo hili.

Alipoulizwa iwapo ameshawishiwa au kushinikizawa na watu au ni ustashi wakae binafsi makamba alisema kuwa yote ni mchanganyiko.

Huwezi kuamka nyumbani na kusema unakwenda kugombea  kuna msukumo wa wapembe wachache ambao ni  lazima ukapime kwa makini kabla  ya kuchukua hatua yoyote alisema.

Nchi nzima unakuta inazunguma uwe rais  lazima upime na chagizo hizo ni za kweli au zinatoka wapi lakini unposikia  hadi viongozi wa dini wanfunzi wa vyuo  unapokwenda  wanakuuliza jambo  hili hilo unatakiwa  kutafakari.

0 Responses to “JANUARY AJITOSA URAIS 2015”

Post a Comment

More to Read