Tuesday, July 22, 2014

PINDA: UCHAGUZI UNASUBIRI HATIMA YA KATIBA MPYA.




Waziri Mkuu, Mizengo Pinda amesema Serikali imeshaanza maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu wa Rais, wabunge na madiwani mwakani lakini tatizo ni Katiba Mpya.
Pinda alitoa kauli hiyo jana katika chuo cha ufundi, Kijiji cha Gonja wakati akiweka jiwe la msingi.

“Je, Katiba hiyo Mpya itapita na kama isipopita je, uchaguzi bado utakuwapo Oktoba au tutausogeza mbele kidogo?” alisema na kuongeza kuwa changamoto kubwa ni pale Ukawa waliposusa.
“Jitihada zinazoendelea hivi sasa ni kuwataka warudi kwa sababu mjadala uko bungeni. Pale ambapo itaonekana tuliteleza tuombane msamaha tusonge mbele”.

“Tubishane lakini tusiwe kikwazo. Kama Ukawa hawatarudi kimsingi hatuna tatizo kubwa kwa sababu Katiba ya sasa ya mwaka 1977 itafanyiwa marekebisho madogo ili itumike katika uchaguzi ujao wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu mwakani ili iweze kutuvusha hapa tulipo,” alisema Pinda bila kutaja aina ya marekebisho yanayokusudiwa.

Pinda alisema ni vyema ikafahamika kuwa chochote kile ambacho wajumbe wa Bunge hilo watakubaliana lazima wananchi watakuwa waamuzi wa mwisho kwa kusema ndiyo au hapana.

0 Responses to “PINDA: UCHAGUZI UNASUBIRI HATIMA YA KATIBA MPYA.”

Post a Comment

More to Read