Sunday, December 8, 2013



                                       TANZANITE KUIVAA AFRIKA KUSINI 

Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu Tanzanite itashuka dimbani Jumamosi hii katika uwanja wa Taifa saa kumi  kukipiga na timu ya Afrka kusini maarufu kama Basetsana katika kufuzu mchujo wa kombe la Dunia kwa wasichana wenye umri wa miaka ishirini (20)

Timu ya Afrika Kusini ya wasichana wenye umri wa chini ya miaka ishirini inaingia dimbani huku ikiwa na majonzi ya kumpoteza Rais wao wa zamani Nelson Mandela. Itajua kama itaendeleza majonzi pamoja na kufungwa au kushinda kwa mechi ya kesho.

Kikosi cha Tanzanite kinachonolewa na Rogasian Kiajage amesema, tumejiandaa, vijana wako vizuri na wanasubiri saa ya mechi tu.



Mechi hiyo itahudhuriwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk, Fenella Mukangera. Viingilio vya mechi hiyo vitakuwa Tsh 1000 kwa viti vya kijani, Blue na Orange, Tsh 2000 ni VIP C,Tsh 5000 VIP B, Tsh10000 ni VIP A tiketi zinapatikana mlangoni.

0 Responses to “ ”

Post a Comment

More to Read