Monday, December 22, 2014

MKUU WA WILAYA YA MBEYA AFUNGUA MAFUNZO YA BENKI YA POSTA KWA WAJASILIAMALI.





Mkuu wa wilaya ya Mbeya Dkt.Dakta Norman Sigala amefungua mafunzo kwa wajasiliamali yanayoendeshwa na Benki ya Posta katika jiji la Mbeya jumatatu ya leo.

Wafanyakazi wa Bank ya Posta wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni Rasmi.





Mkuu wa wilaya ya Mbeya/mgeni rasmi Dakta Norman Sigala amefungua mafunzo kwa wajasiliamali yanayoendeshwa na Benki ya Posta katika jiji la Mbeya jumatatu ya leo.

Akifungua mafunzo hayo mbele ya wajasiliamali takribani 200,viongozi wa benki ya Posta na waandishi wa habari,Mgeni rasmi ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Mbeya Dakta Norman Sigala amesema kuwa watendaji katika mabenki wanatakiwa kurekebisha riba, kutoa mafunzo kwa wajasiliamali na hata kuwa na wataalamu wa kufanya michanganuo ya mawazo wa wateja ili kuwafanya wateja wao kunufaika na mikopo yao.

Pamoja na hayo, Dakta Norman Sigala amewasihi wajasiliamali kuhamasisha amani kwa watu wote kwani pasipo kuwepo amani hakuna shughuli yoyote ya kibiashara itakayofanyika pamoja na kuwapinga viongozi wa kidini na kisiasa wanaochochea mvunjiko wa amani.

Akihitimisha hotuba yake fupi ya ufunguzi, bw. Dakta Norman Sigala ambaye pia ni mjasiliamali wa siku nyingi aliyeanza kukopa katika mabenki tangu mwaka 1994, amewashauri wajasilia mali kukopa bila woga lakini kwa kuzingatia nidhamu ya biashara na urejeshaji wa mikopo hiyo.

Benki ya Posta inaendelea na mfululizo wa mafunzo kwa wajasiliamali nchi nzima ambapo kesho mafunzo hayo yatatolewa kwa wajasiliamali wa mji wa Tunduma katika wilaya ya Momba mkoani Mbeya.

0 Responses to “MKUU WA WILAYA YA MBEYA AFUNGUA MAFUNZO YA BENKI YA POSTA KWA WAJASILIAMALI.”

Post a Comment

More to Read