Monday, December 22, 2014
TISA( 9) WAFA KATIKA AJALI YA BASI TUNDUMA MBEYA.
Do you like this story?
Kamanda wa polisi Mkoa wa Mbeya Bw Ahamed Msangi |
Na EmanuelMadafa
WATU 9 wamepoteza maisha papo hapo na wengine 13
kujeruhiwa mkoani Mbeya baada ya basi ndogo ya abiria aina ya Coaster
lenye namba za usajili T 203 ARZ kuyagonga magari mawili.
Akizungumzablog hii Kamanda
wa polisi wa Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi aliyekuwa katika eneo la tukio, amesema tukio hilo lilitokea majira
ya saa nane za mchana katika eneo la Sengula Kata ya Tunduma Wilayani Momba.
Amewataja waliofariki katika ajali ya
Tunduma kuwa ni Amina Michael,Neema Almasi, Rose Hezron Halele, wakazi wa
Tunduma, Hebeli Mkilimi Mkazi wa Ileje, Thomasi Simfukwe mkazi wa Hamwelo
Mbozi, Exavery Mubiso mkazi wa Ukwile Mbozi na watu wengine watatu
hawajatambulika ambao walipata ajali katika eneo la Sogea Tunduma na Hamad
Imani Masawe mkazi wa Dar Es salaam na kwamba wote ni watu wazima.
Amesema majeruhi katika ajali ya Sogea Tunduma walikuwa 24 ,12 kati yao wametibiwa na kuruhusiwa kurudi makwao, wane wamelazwa hospitalini hapo na 12 wamekimbizwa hospitali ya rufaa kwa matibabu zaidi.
Amewataja waliolazwa kuwa ni Vicky Michael Ngowi (33), Grace Mgimba (33), Sharifa Jemadari(25), Christina Mtende(31), Zainab Jamadin (1), wote wakazi wa Tunduma, Eneth Mkomanga(17) mkazi wa Ilembo ambao wamepelekwa hospitali ya Rufaa Mbeya.
Wengine ni Jackson Mwashambwa mkazi wa Mlangali, Cyprian Mwananzumi (50) mkazi wa Njombe, Siamini Sichenje(30) Emmanuel kamwela(9)mkazi wa Tunduma, na John Zumba mkazi wa Mlowo.

Kamanda, Msangi alisema kuwa Coaster hiyo ikiwa inaendeshwa
na dereva asiyefahamika ilikuwa likitokea Mbeya kwenda Tunduma hivyo kukutana
na maswahiba hayo wakati likijaribu kulipita Lory la mizigo aina ya Tata lenye
namba za usajili T 789 AZL lililokuwa mbele yake.
Alisema, Coaster hiyo ikiwa inapandisha kilima kidogo
kilichopo kwenye eneo hilo na kujaribu kulipita Lory, mbele yake lilitokea basi
kubwa la abiria ambalo lilikuwa likitokea Sumbawanga kuelekea Mbeya, hivyo
dereva wa Coaster kushindwa pa kukimbilia na kuhamua kulipenyeza gari hilo
katikati ya magari hayo mawili.
Kwa mujibu wa Kamanda Msangi, inadaiwa kwamba Coaster
hiyo ilienda kuligonga Lory la mizigo upande wa kulia na upande wa kushoto
kuliparamia basi kubwa na kusababisha vifo vya watu sita na kujeruhi 13.
Aidha, alisema kuwa miili ya marehemu hao imehifadhiwa
katika hospitali ya serikali ya Tunduma na majeruhi wanaendelea kupatiwa
matibabu katika hospitali ya Wilaya ya Mbozi na Tunduma.
.
Mwish
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “TISA( 9) WAFA KATIKA AJALI YA BASI TUNDUMA MBEYA.”
Post a Comment