Friday, September 15, 2017
WATU WANNE WAFARIKI KATIKA AJALI MBEYA
Do you like this story?
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Naibu Kamishina
wa Polisi MOHAMMED R. MPINGA
|
Mwonekano wa Gari aina ya Coaster iliyopata ajali. |
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 15.09.2017.
Jeshi
la Polisi Mkoa wa Mbeya limeendelea kufanya misako, operesheni na doria zenye
tija katika maeneo mbalimbali ili kudhibiti uhalifu na wahalifu na limekuwa likishirikiana
na wananchi na wadau wengine katika jitihada hizo za kukabiliana na uhalifu na
wahalifu na kupata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kupungua kwa matukio
makubwa ya uhalifu.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaongeza
jitihada za kuzuia na kupunguza matukio ya ajali za barabarani kwa kuhakikisha madereva
na watumiaji wengine wa barabara wanafuata sheria na alama za usalama
Barabarani. Aidha kumekuwa na ajali 01 ya vifo kama ifuatavyo:-
Mnamo tarehe 14.09.2017 majira ya saa
19:45 usiku huko eneo la Mlima Iwambi, Kata ya Songwe, Tarafa ya Usongwe,
Wilaya ya Mbeya Vijijini, Mkoa wa Mbeya katika barabara kuu ya Mbeya kwenda
Tunduma, kulitokea ajali iliyohusisha magari matano yenye namba za usajili T. 231 BME aina ya Tipper ikiendeshwa
na dereva FRED MWAKALINGA [33] Mkazi
wa Itiji - Mbeya ikitokea Mbeya mjini kwenda Mbalizi, Gari yenye namba za
usajili T. 515 ARE aina ya Fuso
iliyokuwa ikiendeshwa na dereva EMMANUEL
JULIUS [29] Mkazi wa Itiji ikitokea Mbalizi kwenda Mbeya mjini, Gari yenye
namba za usajili T.126 DJZ aina ya Fuso
basi iliyokuwa ikiendeshwa na AMOS
MWAIKAJA @ CHODO [40] Mkazi wa
Kagera – Soweto, Gari yenye namba za usajili BCA 8730 na tela BCA 8733
ikiendeshwa na EVANS MUSONDA [39] raia
wa Zambia na Gari yenye namba za usajili T.570
CKC aina ya Toyota dyana ikiendeshwa na dereva AMOS BENSON pamoja na Pikipiki moja ambayo haijafahamika namba zake
za usajili ikiendeshwa na dereva aitwaye JANIA
JACKOBO @ SANGA [27] Mkazi wa Iwambi.
Katika
ajali hiyo watu wanne walifariki dunia ambao ni dereva wa Gari yenye namba za
usajili T.570 CKC AMOS BENSON, mwendesha
Pikipiki ambayo bado hajafahamika namba zake za usajili aitwaye JANIA JACKOBO @ SANGA [27] Mkazi wa
Iwambi, dereva wa Gari lenye namba za usajili BCA 8730/BCA 8733 EVANS MUSONDA [39] raia wa Zambia na Mwanamke
mmoja ambaye bado hajafahamika ambaye alikuwa abiria kwenye Gari yenye namba za
usajili T.570 CKC Toyota Dyana.
Aidha
katika ajali hiyo, watu wengine tisa walijeruhiwa kati yao wanaume ni wanne na
wanawake watano. Aidha kati ya majeruhi hao, wawili wamelazwa Hospitali ya
Rufaa Mbeya na saba wamelazwa Hospitali Teule Ifisi - Mbalizi. Chanzo cha ajali
kinachunguzwa hata hivyo inahisiwa kuwa dereva wa lori alikosa umakini na
kuanza kugonga magari mengine ambaye pia amepoteza maisha katika ajali hiyo.
Upelelezi unaendelea ili kubaini chanzo halisi cha ajali na dereva aliyehusika.
WITO:
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mbeya Naibu Kamishina wa Polisi MOHAMMED R. MPINGA anatoa wito kwa Madereva kuwa makini wanapotumia
vyombo ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika. Aidha Kamanda MPINGA anawataka madereva kufuata,
kuheshimu na kuzingatia sheria na alama za barabarani ili kuepuka ajali.
Imesainiwa na:
[MOHAMMED R.
MPINGA - DCP]
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “WATU WANNE WAFARIKI KATIKA AJALI MBEYA ”
Post a Comment