Monday, December 22, 2014
BREAKING NEWS: JOHNSON LUKAZA NA MWESIGWA LUKAZA WASHINDA KESI DHIDI YA EPA
Do you like this story?
JOHNSON LUKAZA WA KESI YA EPA ASHINDA KESI |
HATIMAYE
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, imemwachilia huru Mwenyekiti
wa Makampuni ya Proin, Johnson Lukaza na mdomo wake Mwesiga Lukaza
waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya wizi wa Sh.Bilioni Sita Katika Akaunti ya
Madeni ya Nje ya Benki Kuu(EPA), baada ya kumuona Hana hatia Katika Kesi
iliyokuwa ikimkabili.
Hukumu hiyo
Imetolewa Jaji wa Mahakama Kuu Edson Mkasimongwa aliyekuwa alisaidia na Hakimu
Mkazi Pamela Mazengo.
Lukaza ambaye
pia ni Mjumbe wa Baraza la Chuo Kikuu cha Bagamoyo (UB) alikuwa akitetewa na
Wakili maarufu nchini Alex Mgongolwa aliyekuwa akisaidiwana na Wakili Alex
Mshumbusi.
Akisoma
hukumu hiyo Jaji Mkasimogwa alisema Kesi hiyo ya Mwaka 2008 , Mahakama
imesikiliza ushahidi wa pande zote mbili Na kupitia vielelezo mbalimbali,
Mahakama yake Imefikia uamuzi wa kuwaachiria huru washitakiwa wote Wawili
kwasababu upande wa jamhuri umeshindwa kuleta ushahidi thabiti ambao
ungeishawishi Mahakama hiyo iwakute na hatia washitakiwa Hao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “BREAKING NEWS: JOHNSON LUKAZA NA MWESIGWA LUKAZA WASHINDA KESI DHIDI YA EPA”
Post a Comment