Saturday, July 5, 2014

RAIS KIKWETE ATAKA UBORA ZAIDI WA BIDHAA ZA TANZANIA.



Rais  Jakaya Kikwete  amewataka wafanyabiashara  nchini kuongeza juhudi za kuongeza ubora zaidi wa bidhaa zao ili ziweze kushindana na  zile za nje ya nchi.

Aidha Rais Kikwete amewapongeza washiriki wa maonesho ya 38 ya  Biashara ya Kimataifa  kwa kuongeza ubora wa bidhaa ambao kila mwaka kumekuwa na tofauti.

Kauli hiyo imetolewa leo na Rais Kikwete  wakati  akitembelea leo  maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea  kwenye viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere jijini Dares Salaam.
“ Maonesho ya mwaka huu yamepiga hatua kubwa kwani kumekuwepo kwa ongezeko la bidhaa, bidhaa zimefungwa vizuri tukiendelea hivi tunaweza kushindana na bidhaa za kimataifa. Pendekezo langu  mimi ni kuendelea kufanya ziwe vizuri zaidi,” alisema Rais Kikwete.

 Akitembelea banda la Jeshi la M,agereza, Rais Kikwete ambapo alijionea uzalishaji wa bidhaa za kilimo, alilitaka jeshil  hilo kutoa elimu kwa wananchi juu ya kilimo bora cha kisasa.
 Katika ziara hiyo Rais Kikwete alitembelea mabanda mbalimbali likiwemo la Wakala wa Mafunzo nje ya nchi. Benki Kuu ya Tanzania, Bidhaa za Tanzaniana mengineyo.

0 Responses to “RAIS KIKWETE ATAKA UBORA ZAIDI WA BIDHAA ZA TANZANIA.”

Post a Comment

More to Read