Thursday, July 3, 2014

TFF,CRDB YATOA SEMINA KWA VIONGOZI WA MPIRA WA MIGUU MBEYA JUU MATUMIZI YA TIKETI ZA KIELEKTRONIKI.


Afisa Habari Shirikisho la Mpira wa Miguu TFF Nchini Boniface Wambura akizungumza katika mafunzo ya siku moja kwa wadau na vingozi wa mpira wa miguu Mkoani Mbeya juu ya Kuanza kwa mfumo mpya wa ununuzi wa Tiketi za Kierekroni jijini


Mmoja wa Maofisa wa Benki ya CRDB akionyesha moja ya mashine itakayotumika katika ununuzi wa Tiketi za Kielektroniki ambapo majaribio ya mashine hizo zinatalajiw akuanza katika mechi ya Mbeya City na Prisons katika uwanja wa sokoine jijini Mbeya


Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini TFF pamoja na Benki ya CRDB wametoa  mafunzo ya matumizi ya tiketi za elektroniki  mkoani Mbeya kwa kushirikisha  wasimamizi wa mechi katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine mbeya  , viongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mbeya (MREFA).

Wengine waliopatiwa mafunzo hayo , meneja wa Uwanja wa Sokoine na msaidizi wake, makatibu wa Tanzania Prisons na Mbeya City, maofisa habari wa Mbeya City na Tanzania Prisons, Ofisa Usalama wa MREFA na wasimamizi wa milangoni (stewards).

Semina hiyo inalengo la kuwanda wadau hao katika kusimamia  mfumohuo utakao anza  na timu  za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) za Mbeya City na Tanzania Prisons kwa mchezo wao wa kirafiki Jumamosi (Julai 5 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.

Akizungumza katika semina hiyo   Ofisa wa mifumo ya kibenki ya  kielektroniki, Kalington Chahe,  toka benki ya CRDB, mfumo huo unatoa fursa kwa kila mtu kupata fursa ya kutazama mechi pasipo kuwa na usumbufu wa aina yoyote katika hususani katika suala la ununuzi a tiketi.

Amesema kwa kila mtu mwenye simu ya mkoni anauwezo wa kununua tiketi hata tano kwa wakati mmoja na kuepuka suala la kulanguliwa na mawakala wasio waaminifu.

“Tumefanya hivyo makusudi kwa kuwa tunaamini kuwa katika familia baba anaweza kununua tiketi tano ambazo ataingia yeye na familia yake isiyozidi watu wane, hivyo kufanya idadi ya watu kutoka familia moja kuwa watano” alifafanua Chahe.

Hata hivyo amesema kuwa hali hiyo haizuii timu kununulia mashabiki wake tiketi za mchezo kwani kutakuwa na utaratibu wake.


Akichangia mada katika mafunzo hayo, mmoja wa washiriki , Charles Mwakipesile, alitoa changamoto juu ya mfumo huo utakavyowezesha timu za majeshi zinazokuwa na mashabiki wake maalumu ambao mara nyingi huingia bure uwanjani.


Mechi hiyo ambayo itakuwa ya kwanza kuchezwa jijini Mbeya katika mfumo wa matumizi ya tiketi za elektroniki kwa washabiki wanaoingia uwanjani itaanza saa 10 kamili jioni.
Kiingilio ni sh. 3,000 kwa majukwaa yote ambapo tiketi zimeanza kuuzwa leo (Julai Mosi mwaka huu).

Wakati huo huo, Afisa Habari wa TFF Boniface Wambura amesema  kutakuwa na utaratibu maalumu kwa waandishi wa habari za michezo kwa ajili ya kuripoti mechi hiyo.

0 Responses to “TFF,CRDB YATOA SEMINA KWA VIONGOZI WA MPIRA WA MIGUU MBEYA JUU MATUMIZI YA TIKETI ZA KIELEKTRONIKI.”

Post a Comment

More to Read