Wednesday, July 23, 2014

WAJAWAZITO WALALA MZUNGU WA NNE KITUO CHA AFYA KAMBARAGE -SHINYANGA.




Vitanda vya wagonjwa vikiwa vimefungwa kwenye mabox kutokana na kukosekana sehemu pa kuviweka kutokana na ufinyu wa wodi pamoja na upungufu.


Wakinamama wajawazito na waliojifungua wakiwa katika wodi moja kwenye kituo cha afya cha Kambarage manispaa ya Shinyanga kutokana na upungufu wa wodi,hali ambayo inaweza kuhatarisha afya zao kwa kuambukizana magonjwa.

Daktari anayesimamia kituo hicho Costantine Hubby alisema
hali hiyo  imesababisha wanawake wajawazito na waliojifungua kulala wawili wawili kitanda kimoja na wengine kulazimika kuweka magodoro sakafuni huku akitaja changamoto nyingine ni kituo kukosa chumba cha upasuaji wa dharura kwa wajawazito wenye uchungu  pingamizi pamoja na kutokuwa na gari la wagonjwa hivyo kusababisha usumbufu mkubwa mgonjwa akiwa amezidiwa hasa wakati wa msimu wa masika mvua zinaponyesha na kuwa katika hatari  iwapo atachelewa kufikishwa kwenye huduma.

0 Responses to “WAJAWAZITO WALALA MZUNGU WA NNE KITUO CHA AFYA KAMBARAGE -SHINYANGA.”

Post a Comment

More to Read