Friday, August 29, 2014

AJALI YAUA KUMI PAPO HAPO NA KUJERUHI WATU SABA ENEO LA MBALIZI MBEYA VIJIJINI.


Mwonekano wa Gari ya aina ya Hice iliyopata ajali Mbalizi Mbeya Vijijini


Askari wa kitengo cha usalama barabarani akiwa anakagua Gari aina ya Toyota hice lililopata Ajari


Moja ya Gari lililopata ajari aina ya Fuso



Majeruhi Neima Ituga akipelekwa wodini baada ya kupatiwa huduma ya kwanza.

Kondakta wa gari  Aina ya Toyota Hice Justin Chaula akikimbizwa kwenye chumba cha X Ray kilichopo katika Hospital Teule ya Ifisi iliyopo Mbeya Vijijini.

(Picha na Fahari News)



WATU 10 wamefariki papo hapo na wengine saba kujeruhiwa katika ajali ya gari dogo la abiria Toyota Hiace  kulivaa Lori aina ya Fuso eneo la Mbalizi lililopo Mbeya vijijini.

Tukio hilo limetokea jana  saa 4:00 asubuhi katika eneo la Mbalizi lililopo Mbeya Vijijini.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi,amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambayo imehusha gari ya abiria  aina ya Toyota Hiace yenye namba za usajili T237, ikitokea Jijini Mbeya kwenda Mbalizi kulivaa  Lori  aina ya Fuso lenye namba za usajili  T 158 CSV lilikuwa likitokea kwenye kituo cha mafuta kilichopo eneo la Mbalizi.

Amesema, waliopoteza katika ajali iyo ni watu 10 miongoni mwao ni dereva wa Hiace aliyetambulika kwa jina la Petro Mngo’ngo na kujeruhi wengine saba na kwamba chanzo cha ajali hiyo kinachunguzwa.

Akizungumza na Fahari News, Muuguzi Mkuu wa  hospitali Teule ya Ifisi,  Sikitu Mbilinyi, amekiri kituo hicho kupokea miili ya marehemu 10 na majeruhi saba na kwamba waliopoteza maisha ni watoto wawili, wanawake wanne na wanaume wanne.

Amesema, majeruhi waliopokelewa  ni wanawake watatu na wanaume wanne kati yao  wanaume wawili na mwanamke mmoja wamekimbizwa katika hospitali ya Rufaa kwa matibabu zaidi.

Muuguzi huyo amesema miili ya marehemu hao imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali hiyo ya Ifisi na kuwataka watu kufika kwenye hospitali hiyo kwa ajili ya kutambua marehemu hao.

Mwisho.


0 Responses to “AJALI YAUA KUMI PAPO HAPO NA KUJERUHI WATU SABA ENEO LA MBALIZI MBEYA VIJIJINI.”

Post a Comment

More to Read