Saturday, August 16, 2014
HOJA MPYA ZALICHANGANYA BUNGE MAALUM.
Do you like this story?
Dodoma. Mapendekezo mapya yanayopelekwa kwenye Kamati za Bunge
Maalumu kwa ajili ya kurekebisha baadhi ya Ibara za Rasimu ya Katiba, yamezua
mivutano mikali kiasi cha baadhi ya sura kuwekwa kiporo au kurukwa na kamati
husika.
Habari
zilizolifikia gazeti hili zinasema mapendekezo hayo ni yale yanayozigusa
taasisi kubwa za nchi, zikiwamo Bunge la Jamhuri ya Muungano na Mahakama,
pamoja na nafasi za Makamu wa Rais.
Katika
baadhi ya kamati yamepelekwa mapendekezo ambayo yanataka Bunge liwe na sehemu
tatu ili kutoa fursa kwa mambo ya Tanzania Bara kujadiliwa bila wabunge kutoka
Zanzibar kuwapo.
“Mapendekezo
yaliyopo ni kwamba wanataka Bunge liwe na sehemu tatu ambazo ni Bunge la
Muungano kwa masuala ya muungano na humohumo linakuwa na sehemu mbili ambazo ni
wabunge wa Zanzibar kwa ajili ya masuala ya Wazanzibari na sehemu ya Tanganyika
kwa ajili ya mambo ya bara,” kilisema chanzo chetu kutoka katika kamati moja ya
Bunge hilo.
Hata
hivyo, habari zinasema baadhi ya wajumbe wa kamati walikosoa pendekezo hilo kwa
maelezo kwamba linashabihiana na muundo wa muungano wa serikali tatu ambao
ulipendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba lakini ukapingwa na baadhi ya
wajumbe wakiongozwa na walio wanachama wa CCM.
Jana
Mwenyekiti wa Kamati Namba 8, Job Ndugai aliwaambia waandishi wa habari kwamba
kamati yake imeshindwa kuafikiana kuhusu muundo wa Bunge la Muungano hivyo
kulazimika kuliacha suala hilo ili kulifanyia uchunguzi kwanza.
“Mbali
na sura ya 5 inayozungumzia uraia pacha ambayo ilitusumbua, lakini pia suala la
Muundo wa Bunge la Muungano na Mahakama ya Muungano vilikuwa tatizo katika
kamati yangu,” alisema Ndugai.
Licha
ya kwamba Ndugai hakuzungumzia suala hilo kwa undani, lakini taarifa
zilizolifikia gazeti hili zinasema muundo wa kuwa na sehemu tatu katika Bunge
moja ndio uliozua mtafaruku kiasi cha kamati hiyo kuliahirisha.
Katika
kamati namba 5, sura ya 10 inayozungumzia suala la Bunge na Mahakama imerukwa.
Mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo alisema: “Tumeamua kuendelea na mambo mengine
kwanza maana hilo limeonekana kuwa ni gumu kwa sasa.”
Habari
zaidi zinasema katika kamati hiyo namba tano, mapendekezo ya kuwapo kwa makamu
wa rais watatu yalizua mjadala mkali kiasi cha kusababisha kuwapo kwa wajumbe
walioamua kuandaa maoni ya wachache.
“Wamekuja
na mapendekezo kwamba awepo Makamu wa Kwanza wa Rais ambaye atakuwa mgombea
mwenza, Makamu wa Pili wa Rais ambaye atakuwa Rais wa Zanzibar na Makamu wa
Tatu wa Rais ambaye ni Waziri Mkuu,” kilisema chanzo chetu kutoka ndani ya
kamati hiyo na kuongeza:
“Lakini
wapo waliokataa kama watano au sita hivi na wameamua kwamba wataandika maoni ya
wachache kwa mujibu wa Kanuni ya 32 (10)”.
Via>Mwananchi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “HOJA MPYA ZALICHANGANYA BUNGE MAALUM.”
Post a Comment