Saturday, August 16, 2014
WATU WAWILI WAFARIKI PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI ILIYOBEBA MAITI 10.
Do you like this story?
Watu wawili wamefariki dunia papo hapo baada ya gari
aina ya Land Cruser ilikuwa imebeba maiti 10 zikitokea hosiptali ya taifa
Muhimbili kwenda hospitali ya St Francis Ifakara kugonga wapanda pikipiki
katika eneo la Mtego wa simba Mikese mkoani Morogoro
Akizungumzia
tukio hilo kwenye eneo la tukio mkuu wa kikosi cha usalama barabarani
Bonifasi Mbao amesema gari hiyo ikiendeshwana dereva Pankrasi Pasco mkazi wa
ifakara iliwagonga wapanda pikipiki Shaban Rajab na Ally Benulo wakazi wa
Mikese na kufariki dunia papo hapo na chanzo cha ajali mwendo kasi na
dereva anashikiliwa na jeshi la polisi, kuhusu maiti 10 zilizokuwemo katika
gari hiyo amesema zilikuwa zikipelekwa hospitli ya St Fancis Ifakar kwa lengo
la kufanya utafiti na mafunzo ambapo wanafanya mawasilino ya kuzifikisha katika
hospitali hiyo.
Nao wananchi
walioshuhudia tukio hilo wameeleleza chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi
huku wakilalamikia matukio ya ajali nyingi katika eneo hilo kutokana na kona na
kuomba serikali kuweka matuta na vibao vya tahadhari.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ WATU WAWILI WAFARIKI PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI ILIYOBEBA MAITI 10. ”
Post a Comment