Tuesday, August 26, 2014

HATARI: MWANAFUNZI ATIWA MBARONI IRINGA KWA TUHUMA ZA KUJIFUNGUA NA KUMUUA MWANAYE KIKATILI


Vena Mtati akitahayari baada ya kutiwa mbaloni na polisi.


MWANAFUNZI wa Chuo cha Uuguzi Chimala wilayani Mbarali, Mkoa wa Mbeya,  Vena Mtati (27) (pichani) anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa kwa madai mazito ya kumuua mtoto wake kwa kumnyonga, kumtumbukiza kwenye mfuko wa rambo na kuutia ndani ya mfuko wa salfeti kisha kuuficha chini ya kitanda

Tukio hilo la kikatili ambalo limewashangaza wengi, hasa ikizingatiwa kuwa mtuhumiwa huyo anajua sheria kwa sababu anajifunza uuguzi, lilijiri Agosti 21, mwaka huu ndani ya nyumba moja iliyopo Kijiweni, Kata ya Mvinjeni mjini hapa.

Kwa mujibu wa shuhuda ambaye anaishi jirani na nyumba inayodaiwa kufanyika mauaji hayo (jina lipo), wiki mbili zilizopita, mtuhumiwa huyo alifika kwenye nyumba hiyo akitokea chuoni akiwa na ujauzito.


“Wiki mbili zilizopita, Vena alifikia kwa rafiki yake anayeitwa Joyce ambaye alikuwa amepangisha katika hiyo nyumba. Vena alikuwa na mimba kubwa, baada ya siku tano tu akajifungua,” kilisema chanzo hicho.

Kikaongeza: “Siku ya tukio, Joyce yeye ambaye ni mwenyeji alitoka kwenda katika shughuli zake, akamuacha Vena akiwa chumbani. Nadhani ndipo aliposhikwa na uchungu, akajifugua mtoto wa kike.

“Ilikuwa asubuhi, sisi tukasikia kelele kutoka kwenye chumba hicho. Zile kelele zilikuwa si za kawaida! Ilikuwa kama vile kuna mtu anakabwa.


“Tuliposikiliza kwa makini, mara sauti ya redio ikaongezwa ili kufanya kelele hizo zisisikike kwa nje. Lakini kwa vile sisi majirani  tulijua kwamba ndani ya chumba kile kuna mjamzito na kelele alizopiga mtoto si za kawaida ndipo tulipomtafuta mwandishi wa habari (hizi),” kilisema chanzo hicho.

0 Responses to “HATARI: MWANAFUNZI ATIWA MBARONI IRINGA KWA TUHUMA ZA KUJIFUNGUA NA KUMUUA MWANAYE KIKATILI ”

Post a Comment

More to Read