Wednesday, August 20, 2014

KIBOKO AVAMIA KIJIJI,WANANCHI WASHINDA JUU YA MITI.




Baadhi ya wakazi wa Kitongoji cha Kashalami Kata ya Mashimboni  wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi wamelazimika kushinda juu ya miti kwa kuhofia kushambuliwa na Kiboko  aliyevamia kijiji hicho  na kuhatarisha uhai wa Wanachi

Kwa mujibu wa Diwani wa Kata hiyo ya Mashimboni  Raphael  Kalinga  tukio hilo  lilitokea hapo Agosti  18 majira ya saa  moja na nusu asubuhi
Akielezea tukio hilo alisema  Kiboko huyo baada  ya kuvamia kijiji hicho  alielekea  kwenye nyumba ya mkazi  mmoja  aitwaye 

Joseph  Kashamakula  ambaye  alinusurika  kushambuliwa na kiboko huyo wakati alipokuwa  akitokea chooni kujisaidia
 Diwani  Kalinga alisema  ndipo Kiboko huyo ambae  alionekana kuwa na hasira 
alipoanza kukanyaga  kanyanga na kuvivunja vyombo vya mwanakijiji huyo ambavyo vilikuwa  nje ya nyumba yake na kuviharibu kabisa  hali ambayo ilimfanya  mwananchi huyo apige mayowe ya kuomba msaada kwa majirani
Majirani walifika kwenye eneo hilo  hata hivyo walilazimika  kutimua mbio  baada ya kiboko huyo  kuanza  kuwafuata  hali ambayo ilipelekea  kukimbia na kisha kupanda juu ya miti kwa kuhofia kushambuliwa na mnyama huyo ambaye aliendelea kuvunja vyombo kwenye nyumba mbalimbali

 Alisema  Kiboko huyo aliendelea kuzunguka kwenye eneo la kijiji hicho na  taarifa za  zilifika kwenye Idara ya Maliasili ya Halmashauri ya  Nsimbo  ambao  walituma Akari wao wa wanyama pori kwenda huko

Baada ya  Askari wa Maliasli kufika kijijini hapo  walianza msako wa kumtafuta kwa kushirikiana na wananchi  ambapo walifanikiwa kumwona na kisha  walimuua kwa kumpiga Risasi  tumboni na kichwani
Diwani   Kalinga  alieleza  baada ya Kiboko kuuwa  wananchi  licha ya hapo awali kumkimbia kiboko huyo  walianza  kugombea  nyama  ya  mnyama huyo  kwa kuchukua  kitoweo cha mboga na  baada ya nusu saa wakawa wamemmaliza.

Na  Walter  Mguluchuma-Mpanda Katavi

0 Responses to “ KIBOKO AVAMIA KIJIJI,WANANCHI WASHINDA JUU YA MITI. ”

Post a Comment

More to Read