Saturday, August 16, 2014
NDEGE YA INDIA ILIYOKUWA NA ABIRIA 280 YASHUKA FUTI 5000 ANGANI BAADA YA RUBANI KUSINZIA.
Do you like this story?
Mamlaka ya anga nchini India
inachunguza tukio la hatari lililotokea Agosti 8, baada ya ndege ya Jet Airways
Boeing 777-300 iliposhuka angani kwa zaidi ya futi 5000 (mita 1500) kutoka
kwenye urefu waliopangiwa kuruka baada ya rubani wake kusinzia.
Tukio hilo lilitokea wakati ndege
hiyo ikifanya safari kutoka Mumbai, India kwenda Brussels, Ubelgiji.
Times of India imeripoti kuwa
rubani aliyekuwa akiongoza ndege hiyo alipumzika kidogo, mapumziko ambayo kwa
viwango vya kimataifa huitwa ‘controlled rest’ kwa zile ndege za masafa marefu.
Safari ya ndege kutoka Mumbai hadi Brussels ni masaa 9.
Rubani msaidizi alitakiwa kuchukua
majukumu yote ya kuongoza ndege kwa wakati huo, lakini inadaiwa rubani huyo wa
kike alisema naye alikuwa busy na tablet ya ndege hivyo hakugundua ndege
ilipoanza kushuka kutoka kwenye urefu wa futi 34,000 iliyotakiwa kuruka wakati
wanapita Uturuki.
Kwa bahati nzuri waongozaji wa
anga wa Uturuki waligundua kuwa ndege hiyo iliyokuwa katika anga lao imeshuka
kwenye urefu (altitude) ambao umepangwa kwaajili ya ndege nyingine, na
kumtaarifu rubani msaidizi arudi kwenye urefu waliopangiwa.
Marubani wote wawili wa ndege hiyo
wamesimamishwa kupisha uchunguzi .
Source: Aljazeera
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ NDEGE YA INDIA ILIYOKUWA NA ABIRIA 280 YASHUKA FUTI 5000 ANGANI BAADA YA RUBANI KUSINZIA.”
Post a Comment