Wednesday, September 17, 2014
ASKARI WAPYA 75 WATUA TABORA, RPC ATOA TAARIFA YA UHALIFU MKOANI HUMO.
Do you like this story?
![]() |
Askari wapya wakimsikiliza Afande Suzan Kaganda alipowapokea mkoani Tabora wakitokea Chuo Cha Polisi Moshi |
Ndugu waandishi wa
habari katika mkoa wetu wa Tabora kumetokea matukio yafuatayo:-
KUPATIKANA NA MADAWA
YADHANIWAYO KUWA YA KULEVYA NA
PIKIPIKI ZA
WIZI: Huko wilaya ya Igunga wamekamatwa watuhumiwa watatu:-
1. WILLY s/o MASHILINGI, 22 yrs, Msukuma,
mkulima na mkazi wa Kahama.
2. SITA
s/o
JILUNGA, 38 yrs, msukuma, mkulima na mkazi wa Nzega.
3. YUSUPH
s/o
MIHAYO, 24yrs, msukuma, mkulima wa mtaa wa Stoo.
4. GILALA
s/o
BULEBA, 35yrs, msukuma, mkulima, mkazi wa Igunga mjini.
wakiwa na madawa ya
kulevya
wanayoyatumiwa kulewesha watu kisha kuwapora pikipiki. Walipohojiwa
walikiri kuhusika na
matukio mbali mbali ya wizi wa pikipiki na kuonesha
pikipiki mbili zenye
namba T 892 CXB, T 522 CQZ, T.914 BUW na T.812 CGU
zote aina ya SANLG
ambazo walizipora huko Puge wilaya
ya Nzega. Juhudi za
kuwatafuta wamiliki halari wa pikipiki hizo zinaendelea.
Watuhumiwa
watafikishwa mahakamani baada ya
upelelezi kukamilika.
KUPATIKANA NA
BHANGI GUNIA MBILI:
Huko wilaya ya Nzega
amekamatwa mtuhumiwa MABULA s/o
EZEKIEL, 23yrs,
Msukuma, mkulima na mkazi wa Ibologero akiwa na bhangi gunia
mbili. Mtuhumiwa
baada ya mahojiano amekiri kuwa ni muuzaji na mtumiaji wa
bhangi.upelelezi
kukamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani
AJALI YA GARI
KUGONGANA NA PIKIPIKI YA MATAIRI MATATU
NA KUSABABISHA VIFO:
Huko kijiji cha Ndono
barabara ya Urambo
gari no. T607 BNV
scania lorry iliyokuwa ikiendeshwa na FUMBA s/o JUMA, 45yrs,
Msambaa, mkazi wa DSM
iligongana na pikipiki ya kubeba mizigo (Guta) REG no.
T153 CWJ SUNLG na
kusababisha vifo vya watu watatu papo hapo ambao ni MAHONA
S/O MUSA WANDEZI,
30yrs, Msukuma, mkazi wa Intika dereva wa pikipiki, HIBHA S/O
LUCAS, 30yrs,
msukuma, mkazi wa Ndono, MABULA S/O MATONGO, 35yrs, msukuma,
mkazi wa Intika
chanzo cha ajali ni uzembe wa dereva wa pikipiki.
AJALI YA GARI
KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU NA KUSABABISHA
KIFO:
Huko maeneo ya
barabara kuu Nzega – Igunga katika kijiji cha Kitangili GARI
T.300 CWB Toyota
Hiace ikiendeshwa na STANSLAUS S/O JOAKIM, 33yrs, Mchaga,
mkazi wa Nzega
ilimgonga mtembea kwa miguu JOKU D/O MBEGESHEN, 32yrs, Msukuma, M/biashara,
mkazi wa Singida na
kufa papo hapo. Chanzo cha ajali ni uzembe wa mtembea kwa
miguu kuvuka barabara
bila tahadhali. Dereva amekamatwa kwa mahojiano zaidi.
Jeshi la Polisi
linazidi kutoa wito kwa
wananchi kuendelea
kushirikiana na Jeshi lao ili kukomesha na kutokomeza
vitendo vyote vya
uhalifu na kuwafichua wahalifu, pia watumiaji wa barabara wafuate
sheria za usalama barabarani.
SUZAN S. KAGANDA
–ACP.
KAMANDA WA
POLISI MKOA WA TABORA.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ASKARI WAPYA 75 WATUA TABORA, RPC ATOA TAARIFA YA UHALIFU MKOANI HUMO.”
Post a Comment