Wednesday, September 17, 2014
FEDHA ZAMGONGANISHA SITTA NA KATIBU WAKE.
Do you like this story?
Dodoma. Kauli
ya Mwenyekiti wa Bunge la Katiba, Samuel Sitta kwamba fedha ambazo zitakuwa
zimeokolewa katika siku 60 za uendeshaji wa Bunge hilo hazitarejeshwa
serikalini, bali zitatafutiwa utaratibu wa namna ya kuzitumia, imemgonganisha
na katibu wake, Yahya Khamis Hamad ambaye amesema “hilo ni jambo la ajabu”.
Sitta alitoa
kauli hiyo juzi usiku wakati akiahirisha Bunge hilo lenye wajumbe 500 baada ya
wajumbe 130 wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kulisusia tangu Aprili 16,
mwaka huu.
Wajumbe hao
wamekuwa wakilipwa posho ya Sh300,000 kwa siku sawa na Sh150 milioni kwa siku
kwa wajumbe wote, huku Serikali ikiwa imetenga Sh20 bilioni kwa ajili ya siku
60 za uendeshaji wa Bunge hilo.
Kauli hiyo ya
Sitta kuwa fedha zitakazookolewa zitatafutiwa utaratibu badala ya kurudishwa
zilikotoka, iliwafanya wajumbe wa Bunge hilo kulipuka kwa furaha na kugonga
meza.
Hata hivyo,
katibu wa Bunge, Yahya Khamis Hamad alishangazwa na kauli hiyo ya Sitta
akisema: “Mimi hayo niliyasikia lakini kwangu pia ni ya ajabu kwa sababu fedha
tulizonazo hazitoshi, sasa hizo za kubaki mimi sijui.”
Katibu huyo
alisema kwa sasa, Wizara ya Fedha inawapa kiasi cha fedha kwa kile tu ambacho
kinahitajika na yeye anatoa taarifa serikalini kwa kiasi kilichotumika. “Mimi
sijui labda yeye anajua sitaki kumsemea,” alisema.
Sitta pia
aliwaeleza wajumbe hao kuwa baada ya kukabidhi Katiba inayopendekezwa, wote
watakabidhiwa cheti na Rais Jakaya Kikwete.
“Cheti hicho
kitakuwa na sahihi ya Rais mwenyewe kwa hiyo tutakaa kidogo kusubirisubiri
Katiba iliyokamilika, haiwezi kuwa ya ovyo ovyo tu lazima iwe na viwango
vizuri,” alisema Sitta na kuongeza:
“Tutachapisha
nakala nyingi kila mmoja aende na waraka huo wa kihistoria nyumbani na itakuwa
ni Katiba bora sana hapa Afrika na Kusini mwa Sahara.”
Mwenyekiti
huyo aliwapiga vijembe viongozi wa Ukawa na makundi mengine yanayopaza sauti
kutaka Bunge hilo lisitishwe ili kuokoa pesa
“Tutamaliza
zoezi hilo Oktoba 3, mwaka huu ili tutoke na Katiba inayopendekezwa kinyume na
wale wanaopiga kelele ovyo bila kuwa na sayansi kichwani eti unaokoa gharama
kwa kusitisha mchakato.
“Mchakato huu
ungesitishwa ina maana utawala ujao, rais ajaye ingembidi kuanza upya na Tume
na aingie tena kwenye Bunge Maalumu la Katiba,” alisema Sitta.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “FEDHA ZAMGONGANISHA SITTA NA KATIBU WAKE.”
Post a Comment