Tuesday, September 16, 2014

KAMPUNI YA SEED CO KUZAWADIA WANAFUNZI MADAWATI 100 YENYE THAMANI YA MIL 15 KATIKA SHINDANO LA SHAMBA DARASA MIKOA YA NYANDA ZA JUU KUSINI.


Kaimu  Meneja wa Seed Co Bw Michael Rikanga akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu mashindano ya Shamba darasa

Kaimu  Meneja wa Seed Co Bw Michael Rikanga akionyesha bango kwa Waandishi wa Habari jinsi ya kushiriki shindano hilo la shamba darasa


Waandishi wa Habari wakiwa makini kumsikiliza kaimu Meneja wa kampuni Seed Co.


Katika kuhakikisha serikali inatimiza azma yake ya kuwakomboa wakulima nchini hususani katika suala la kilimo bora cha kibiashara  taasisi binafsi zinazojiuhusisha na shughuli ya usambazaji  wa  mbegu bora za kilimo zimeendelea na harakati za kuisaidia serikali katika suala hilo.

Hatua hiyo ni pamoja na kutoa elimu pamoja na kusambaza pembejeo bora za kilimo zenye kukidhi mahitaji ya mkulima.
Kutokana na hali hiyo kampuni ya Seed  Co imezindua shindano  rasmi la mashamba darasa  kwa shule za Msingi Tanzania ambazo zitaanza mchakato wa kulima shamba darasa  kwa kufuata kanuni bora za kilimo cha kisasa .

Akizungumza jijini Mbeya Kaimu meneja wa Kampuni hiyo Kanda ya Nyanda za juu Kusini Ndugu Michael Rikanga amesema  shindano hilo ni mahususi kwa shule za msingi za Mbeya  Iringa Njombe na Ruvuma pamoja na Rukwa na Katavi ambapo shindano hilo linatalajiwa kuanza msimu mpya wa kilimo  .

Amesema kwa shule itakayokuwa imelima shamba darasa zuri kwa kuzingatia misingi yote ya kilimo bora cha kisasa itajishindia zawadi kubwa ya madawati yenye thamani ya shilingi mili15.

Amesema  pamoja na  zawadi hiyo ya madati kwa mshindi wa kwanza pia mshindi atapatiwa  sare za michezo  madaftari na kalamu za kuandikia pamoja na mwalimu wa somo la kilimo kupatiwa simu ya mkononi.

Amesema ili kushiriki mwanafunzi au mwalimu wanatakiwa kutembelea maduka ya mawaka maalum waliothibitishwa na Kampuni hiyo ya Seed Co ili kujisajili katika shindano hilo.

Hata hivyo Meneja huyo amesema kuwa katika hatua za uandaaji na usimamizi wa shamba darasa Kampuni hiyo itatoa pemebejeo zote zitakazohitajika  ikiwa ni pamoja na mbegu za mahindi mbolea ya kupandia na kukuzia .

Mahitaji  mengine ni pamoja na madawa ya kupulizia iwapo iwapo mazao yataonyesha dalili za kushambuliwa na wadudu waharibifu.

Lengo la kampeni hiyo kufundisha kilimo  kwa njia ya vitendo  kwa wanafunzi  wa shule za msingi sanjali na kutoa  nafasi kwa wanafunzi kujishindia zawadi kutoka katika kampuni hiyo ya Seed Co Tanzania Limited.

0 Responses to “KAMPUNI YA SEED CO KUZAWADIA WANAFUNZI MADAWATI 100 YENYE THAMANI YA MIL 15 KATIKA SHINDANO LA SHAMBA DARASA MIKOA YA NYANDA ZA JUU KUSINI.”

Post a Comment

More to Read