Thursday, September 4, 2014

MBEYA CITY KUJIPIMA UBAVU NA BIG BULLETS YA MALAWI




Ili kujiimarisha zaidi kuelekea msimu mpya wa ligi kuu Tanzania Bara, klabu ya Mbeya City inataraji kucheza michezo miwili ya kimataifa ya kirafiki kabla ya kuanza kwa msimu mpya Septemba 20 ambapo timu hiyo iliyomaliza katika nafasi ya tatu msimu uliopita itafungua dimba dhidi ya ' Maafande'  wa JKT Ruvu katika uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Kocha mkuu wa timu hiyo, Juma Mwambusi ameuagiza uongozi wa timu hiyo kumtafutia michezo miwili dhidi ya klabu za Malawi.

Big Bullets ni klabu kongwe nchini Malawi na Kusini mwa bara la Afrika itacheza na City katika mchezo wa kwanza wa kimataifa.

 " Nimeuambia uongozi wangu nahitaji mechi mbili ngumu za kimataifa na timu kutoka nchini Malawi. Tunataraji kucheza na Big Bullets ya Malawi ili kujiimarisha zaidi kabla ya kuanza kwa msimu mpya" alisema, Mwambusi.

City imefanikiwa kuwabakisha kikosini wachezaji wake nyota kama, Paul Nongwa, Saad Kipanga, Hassan Mwasapili, na golikipa, David Baruani licha ya wachezaji hao kuwaniwa na timu kubwa katika dirisha la usajili.

Mwagane Yeya, Eric Banda wataungana na nyota mpya, Themi Felix kuifanya timu hiyo kuendelea kuwa bora katika msimu wake wa pili katika ligi ya Tanzania Bara.

0 Responses to “MBEYA CITY KUJIPIMA UBAVU NA BIG BULLETS YA MALAWI”

Post a Comment

More to Read