Thursday, January 21, 2016
DAWASCO YATANGAZA KUZIMA KWA MTAMBO WA MAJI WA RUVU CHINI KWA SIKU MBILI
Do you like this story?
Afisa Uhusiano
wa Shirika la Maji Safi na Majitaka Dar es salaam (DAWASCO), Everlasting Lyaro,
akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) wakati akitoa taarifa ya kuzimwa kwa
Mtambo wa kuzalisha Maji wa Ruvu Chini kwa wastani wa Saa 48 kwa siku za
Jumamosi 23/01/2016 na Jumapili 24/01/2016
Mtambo wa Ruvu
Chini utazimwa ili kuruhusu Mkandarasi Kuunganisha bomba Jipya na Bomba la
zamani katika tanki la Maji Wazo- Tegeta. Zoezi hili linaashiria kuanza
kukamilika kwa upanuzi wa Mtambo wa Maji wa Ruvu Chini ambapo Shirika
linakusudia kuzalisha Maji mapya toka kiwango cha sasa cha cubic za ujazo
182,000 hadi cubic 270,000 kwa siku kuanzia mwezi Februari 2016 na Kuondoa
kabisa tatizo la Maji kwa maeneo yanayohudumiwa na Mtambo wa Ruvu Chini.
Kuzimwa Kwa
mtambo wa Ruvu Chini kutapelekea maeneo yafuatayo katika Jiji kukosa Maji:
. MJI WA
BAGAMOYO VIJIJI VYA ZINGA, KEREGE NA MAPINGA, BUNJU, BOKO, TEGETA, KUNDUCHI,
SALASALA, JANGWANI, MBEZI BEACH NA KAWE.
Maeneo Mengine
ni : MLALAKUWA, MWENGE, MIKOCHENI, MSASANI, SINZA, KIJITONYAMA, KINONDONI,
OYSTERBAY, MAGOMENI, UPANGA, KARIAKOO, CITY CENTRE, ILALA, UBUNGO MAZIWA,
KIGOGO, MBURAHATI, HOSPITALI YA RUFAA MUHIMBILI, BUGURUNI, CHANGOMBE NA KEKO.
WANANCHI
MNASHAURIWA KUHIFADHI MAJI NA KUYATUMIA KWA MATUMIZI YA LAZIMA.
Wasiliana nasi
kupitia kituo cha huduma kwa wateja 022-2194800 au 0800110064 (BURE)
DAWASCO
INAWAOMBA RADHI WANANCHI KWA USUMBUFU UTAKAOJITOKEZA.
IMETOLEWA NA
OFISI YA UHUSIANO
DAWASCO-MAKAO
MAKUU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “DAWASCO YATANGAZA KUZIMA KWA MTAMBO WA MAJI WA RUVU CHINI KWA SIKU MBILI ”
Post a Comment