Thursday, January 21, 2016
WAZIRI MKUU MSTAAFU, MIZENGO PINDA AWAFUNDA WABUNDE WA CCM.......AWATAKA KUJENGA HOJA VIZURI ILI KUWAKABILI WABUNGE WA UPINZANI.
Do you like this story?
WAZIRI Mkuu
mstaafu, Mizengo Pinda amewataka wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kujenga
hoja vizuri katika Bunge linalotarajia kuanza vikao vyake wiki ijayo mjini
Dodoma, kwa kuwa wabunge wa vyama vya upinzani wameongezeka bungeni.
Hayo yalisemwa
jana Dar es Salaam na Pinda, baada ya kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti
Maalumu, Leticia Nyerere, aliyefariki akiwa Maryland nchini Marekani akipatiwa
matibabu.
Akizungumzia
Bunge la sasa, Pinda aliwashauri wabunge wanaounda Bunge hilo ambao wengi wao
ni vijana, kuzingatia maslahi ya taifa na sio itikadi za vyama vyao na
kuwasisitiza wabunge wa CCM, kujipanga na kwenda na hoja.
“Kila
upande ujiandae kwenye kuwasilisha hoja, kuna ongezeko la wabunge wa upinzani,
sasa wabunge wa CCM ni lazima nao wajipange na kujenga hoja vizuri,” alisema Pinda.
Alisema kwa mtazamo wake, Bunge ni zuri na sio la mivutano kwa kuwa kila mmoja amejipanga kuwasilisha hoja zitakazomgusa mwananchi kwa lengo la kumsaidia.
Alisema kwa mtazamo wake, Bunge ni zuri na sio la mivutano kwa kuwa kila mmoja amejipanga kuwasilisha hoja zitakazomgusa mwananchi kwa lengo la kumsaidia.
Akizungumzia
utawala wa Awamu ya Tano wa Rais John Magufuli, Pinda alisema kila zama zina
kitabu chake; na kwa utawala wa Rais Magufuli ameanza vizuri na kuomba
Watanzania kumuunga mkono ili kufanikisha azma ya maendeleo ya taifa.
Alisema katika
uongozi wake, ndio muda wa kuhakikisha Dira ya Taifa ya Maendeleo inayoisha
baada ya miaka 10 ijayo, inapaswa kuwa imetekelezwa, hivyo hatua mbalimbali
anazozifanya rais, ikiwa ni pamoja na kubana matumizi, ni mambo muhimu.
“Hatua
zinazofanywa na Rais Magufuli ni za msingi katika kuhakikisha dira ya Taifa ya
Maendeleo inatekelezwa, ni vyema Watanzania wote tumuunge mkono juhudi zake”, alisema Waziri Mkuu mstaafu Pinda.
Mpekuzi blog
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “WAZIRI MKUU MSTAAFU, MIZENGO PINDA AWAFUNDA WABUNDE WA CCM.......AWATAKA KUJENGA HOJA VIZURI ILI KUWAKABILI WABUNGE WA UPINZANI.”
Post a Comment