Thursday, September 18, 2014
MWANAFUNZI WA KIDATO CHA TANO AJINYONGA AKIWA HOSPITALI....CHANZO CHA KUJINYOGA NI KULAZWA HOSPITALINI HAPO BILAVIPIMO.
Do you like this story?
Katika hali isiyotarajiwa, mwanafunzi wa Kidato cha Tano katika Shule ya Sekondari ya Wavulana Ihungo Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera, Ezra Gerald (19), amejinyonga hadi kufa kwa kutumia shuka ya hospitali, alikokuwa amelazwa kwa kile kinachoeleza alikuwa anasumbuliwa na homa ya matumbo.
Hata hivyo, ujumbe
ulioachwa na marehemu huyo unaonesha alichukua uamuzi huo, kutokana na
kuchukizwa na uamuzi wa daktari aliyemhudumia wa kumlaza ili atibiwe ugonjwa
ambao hakuwa anaumwa.
Aidha, katika ujumbe
huo imeelezwa alichukizwa na kitendo cha kupotezewa muda hospitalini wakati
wenzake wakiendelea na masomo.
Tukio hilo
limethibitishwa na Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Kagera, Gilles Muroto
aliyesema mwanafunzi huo alijinyonga Septemba 16 mwaka huu saa moja asubuhi.
Alisema mwili wake
uligundulika ukining’inia kwenye mti uliopo maeneo ya hospitali hiyo na
alipopekuliwa katika mifuko ya suruali yake, zilionekana karatasi mbili, moja
ikiwa na ujumbe uliosomeka; “Haiwezekani
binadamu kuhudumiwa kama mbwa, yaani nafika hospitali najieleza hali yangu
halafu daktari ananiandikia kulazwa bila kupima, sasa sijui wanatibu nini?
“Kwa kweli siwezi kuvumilia wenzangu
wanasoma halafu mimi nimekalishwa tu hapa hospitali bila kujua wananitibu nini,
inaniuma sana mpaka nafikia hatua hii ya kujiondoa duniani kwa sababu naona
watu wanachezea ndoto zangu, mimi siwezi kuona ndoto yangu inazimwa wakati
natakiwa niwepo shuleni nikamilishe ndoto zangu “mjitahidi tukutane mbinguni
“Respect My Family and Brother Henry.”
Kamanda Muroto
amesema hakuna aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo, lakini polisi wanaendelea
na uchunguzi.
Inaelezwa mwanafunzi
huyo aliyetajwa kuwa ni mwenyeji wa mkoa wa Tabora, alilazwa hospitalini hapo
tangu Septemba 11 mwaka huu.
Kwa mujibu wa Katibu
wa Hospitali ya Mkoa wa Kagera, Benges Justus, tukio hilo lilitokea Septemba
16, mwaka huu, siku moja baada ya mgonjwa huyo kulazwa.
Alisema baada ya
mwanafunzi huyo kupokelewa hospitalini hapo, alifanyiwa vipimo vyote vya kitabibu
na kugundulika anasumbuliwa na malaria, ndipo akaanzishiwa tiba ya ugonjwa huo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MWANAFUNZI WA KIDATO CHA TANO AJINYONGA AKIWA HOSPITALI....CHANZO CHA KUJINYOGA NI KULAZWA HOSPITALINI HAPO BILAVIPIMO.”
Post a Comment