Monday, September 22, 2014
TANESCO MBEYA YAZIDI KULA SAHANI MOJA NA VISHOKA.
Do you like this story?
|
Mkuu wa Kitengo cha Usalama Tanesco
Mkoa wa Mbeya Bw.Cyprian Lugazia akiwa katika moja ya majukumu yake ya kukamata
wahujumu wa shirika hilo
|
WANAWAKE wawili wanashikiliwa na
Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) Mkoa wa Mbeya, kwa tuhuma za kuhusika na
uuzaji na usambazaji wa mafuta ya Transfoma.
Wanawake hao, ambao ni wakazi wa
eneo la Ilomba lililopo Jijini Mbeya, walikamatwa jana majira ya saa mbili usiku,
wakiwa na lita 10 za mafuta hayo, wakitafuta wateja wa kuwauzia.
Kwa mjibu wa taarifa kutoka kwa Mkuu
wa Kitengo cha Usalama cha Tanesco Mkoa wa Mbeya,Cyprian Lugazia aliwataja
wanawake hao kuwa ni Grace Jeremia maharufu kwa jina la (Mama Matha) ambaye ni
muuzaji mzoefu na Sera Zakaria.
Aidha, Afisa huyo, amesema
watuhumiwa hao walikutwa na madumu hayo mawili ya lita tano kila moja
na kuwa mpaka sasa maofisa wa shirika hilo wanaendeleza msako mkali dhidi
ya watu wengine ambao wamekuwa wakilihujumu shirika hilo na kusababisha hasara
kubwa kwa serikali.
“Watuhumiwa hawa watafikishwa
mahakamani mara uchunguzi wa polisi kwa kushirikiana na maofisa wa shirika
utakapokamilika,”alisema.
Kwa upande wake Meneja wa Tanesco
Mkoa wa Mbeya Mhandisi Amosi Maganga, amesema mafanikio ya kukamatwa kwa
watuhumia hao yametokana na ushirikiano unaondelea baina ya shirika hilo na
wananchi ambao wamekuwa wakitoa taarifa za watu ambao wamekuwa wakilihujumu
shirika kwa kujihusisha na vitendo vya wizi wa mafuta pamoja na umeme.
Amesema, shirika limekuwa likiingia
hasara kubwa katika upotevu wa mafuta hayo ya Transfoma ambapo ndi chanzo
kikubwa cha kusababisha kuungua kwa transfoma hizo, hali inayochangia baadhi ya
wanachi kushindwa kupata huduma hiyo ya umeme.
“Ukiangalia katika kipindi cha miezi
sita shirika limepata hasara ya shilingi bilioni moja, hivyo ni vema wananchi
wakaendelea kutoa ushirikiano ili watu hawa wakamatwe na kuchukuliwa hatua za
kisheria,”alisema.
Hata hivyo, ametoa wito kwa wananchi
kuendelea kutoa taarifa na kuwa kwa yeyote atakayefanikisha kukamatwa kwa
wahusika atapewa zawadi nono.
Mei 20 mwaka huu Tanesco Mkoa wa
Mbeya, lilimkamata Mwantika likimtuhumu kujiunganishia umeme kinyemela na
majirani zake na tayari amefikishwa mahakamani.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


.gif)

0 Responses to “TANESCO MBEYA YAZIDI KULA SAHANI MOJA NA VISHOKA.”
Post a Comment