Monday, September 22, 2014
LOUIS VAV GAAL AGEUKA MBOGO KWA WACHEZAJI WA MANCHESTER UNITED..AFOKA USIPIME!
Do you like this story?
![]() |
| Wachezaji wa United wakishangilia bao la Ander Herrera lililowafanya wawe mbele kwa mabao 3-1 |
![]() |
| Louis van Gaal na Ryan Giggs walioneka kushitushwa na kipigo dhidi ya Leicester |
IMETAARIFIWA kuwa
Louis van Gaal aliwacharukia wachezaji wa Manchester United kwenye vyumba vya
kubadilishia nguo kufuatia kipigo cha 5-3 kutoka kwa Leicester.
Van Gaal aligeuka
mbogo akiwalaumu wachezaji wake kwa kupoteza uongozi wa 3-1 na kumaliza mechi
kwa kipigo kizito.
Kocha huyo mwenye
heshima ya kutokuwa na hasira na wachezaji wake, aliwakalipia waziwazi baada ya
kufungwa kwa mara ya pili katika michuano ya ligi kuu England.
United walipata kipigo cha aibu
na kumuacha Van Gaal na hasira za ajabu.
Van Gaal alikuwa na Radamel
Falcao, Wayne Rooney na Van Persie katika kikosi kilichoanza, lakini baadaye
alilalamika akisema: "Tuna wachezaji wengi ambao hawatafuti magoli."
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


.gif)



0 Responses to “LOUIS VAV GAAL AGEUKA MBOGO KWA WACHEZAJI WA MANCHESTER UNITED..AFOKA USIPIME!”
Post a Comment