Wednesday, October 8, 2014
SERIKALI YAONDOA ZUIO LA MIKUTANO YA VYAMA VYA SIASA KATIKA MIKOA YA LINDI NA MTWARA.
Do you like this story?
Serikali
imeondoa zuio la mikutano ya Vyama vya Siasa lililokuwa limetangazwa mwezi Mei
mwaka juzi kuzuia mikutano hiyo kufanyika katika mikoa ya Lindi na Mtwara.
Zuio
hilo limeondolewa leo na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mathias Chikawe.
Mikutano
hiyo ilizuiliwa kutokana na vurugu za wananchi waliokuwa wakipinga ujenzi wa
mradi wa bomba la gesi kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam hali iliyosababisha
kuvunjika kwa amani na utulivu katika mikoa hiyo.
Katika
vurugu hizo, watu kadhaa walipoteza maisha na wengine kujeruhiwa huku magari na
nyumba zikichomwa moto.
Hatua
hii ya sasa imechukuliwa baada ya Serikali kuridhika kuwa hali na amani na
utulivu imerejea katika mikoa hiyo na kuwa mikutano hiyo sasa inaweza kuendelea
kwa kufuata sheria na utaratibu uliowekwa.
Aidha
Jeshi la Polisi litaendelea kutoa ushirikiano katika uendeshaji wa mikutano ya
kisiasa inayoendelea katika maeneo mbalimbali nchini na kuwa vibali vya
mikutano vitaendelea kutolewa kufuatana na mazingira yatakayokuwepo katika eneo
ambapo Chama husika kitakuwa kimeomba kibali.
Ni
matumaini ya Serikali kuwa Vyama vya Siasa vitatumia fursa hii kuendesha
mikutano yao kwa amani na utulivu kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kama
taratibu za uendeshaji wa mikutano hiyo zinavyoelekeza.
Imetolewa
na:
Isaac
J. Nantanga
MSEMAJI
WIZARA
YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
07/10/2014
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


.gif)


0 Responses to “SERIKALI YAONDOA ZUIO LA MIKUTANO YA VYAMA VYA SIASA KATIKA MIKOA YA LINDI NA MTWARA.”
Post a Comment