Monday, November 10, 2014

AZAM FC WAPOKEA KIFAA KIPYA KUTOKA IVORY COAST.


 Serges Pascal Wawa Sfondo akitokea klabu ya El Mereikh ya nchini Sudan.


Unaambiwa Azam FC wameshamshusha bongo huyu mkali wa soka kama inavyoonekana kwenye picha na wanatarajia kumsajili  beki huyu wa Ivory Coast aitwae Serges Pascal Wawa Sfondo akitokea klabu ya El Mereikh ya nchini Sudan.
Ameingia na ndege ya saa nane usiku wa kuamkia November 10 2014 ambapo millardayo.com na AyoTV ilikua kwenye uwanja wa ndege Dar es salaam kuhakikisha stori haipiti bilabila.

Imeshindikana kumpata sana Pascal akizungumza kwenye interview kwa sababu hajui kuzungumza lugha nyingine tofauti na za Kiarabu na Kifaransa alizozizoea.

Club alizozichezea ni ASEC Mimomas kuanzia mwaka 2003 mpaka 2010 alipojiunga na Al-Merrikh ya Sudan ambapo kwa mujibu wa mtandao, hajawahi kuzifungia timu hizi goli lolote.

Umri wake ni miaka 28, alizaliwa January 1 1986.

millardayo.com  

0 Responses to “AZAM FC WAPOKEA KIFAA KIPYA KUTOKA IVORY COAST.”

Post a Comment

More to Read