Monday, November 10, 2014

UMEIPATA HII YA HALI YA RAIS KIKWETE BAADA YA KUFANYIWA UPASUAJI HUKO MAREKANI




Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe Liberata Mulamula aliyekwenda kumjulia hali katika hospitali ya John Hopkins iliyopo Baltimore, Maryland, nchini Marekani, jana Jumapili, siku moja baada ya kufanyiwa upasuaji wa Tezi Dume.

Habari kutoka hospitalini hapo zinasema Rais Kikwete anaendelea vyema na leo asubuhi alianza mazoezi ya kutembea, kuashiria kwamba mambo yote ni mswano. 

Tutaendelea kwuashirikisha taarifa ya maendeleo yake
mara kwa mara. Tuzidi kumuombea apate nafuu haraka ili arejee nyumbani kulijenga Taifa.

PICHA NA IKULU

0 Responses to “UMEIPATA HII YA HALI YA RAIS KIKWETE BAADA YA KUFANYIWA UPASUAJI HUKO MAREKANI ”

Post a Comment

More to Read