Friday, November 7, 2014

AJALI MBAYA YAUA DEREVA WA NSSF NA MENEJA WAKE MBEYA





Trekta likivuta kichwa cha lori hilo ilikuweza kumtoa dereva aliyeminywa(Picha kwisani ya Mkinda.blogspot.com)



Na Bosco Nyambege,MBOZI
Watu wawili wamefariki dunia wilayani mbozi mkoani Mbeya na mmoja kunusurika katika ajali ya barabarani iliyotokea eneo la Old Vwawa darajani na lililohusisha gari aina ya Toyota Land Grusser mali ya shirika la NSSF tawi la Mbozi na lori la mafuta.

Mashuhuda wa tukio hilo wamesema chanzo ya ajali hiyo ni gari aina ya Lori yenye namba za usajili T.830 CQE  lililokuwa likitokea Mbeya kuelekea Tunduma  alipokuwa over take msafara wa harusi na ndipo alipogongana uso kwa uso na gari hilo la NSSF lenye namba za usajili SU 36276.

Akizungumzia ajali hiyo kwa niaba ya mganga mkuu wa hospitali ya Serikali ya Mbozi Dr Elekizemba Alfan amesema wamepokea miili ya maita wawili wafanyakazi wa shirika la NSSF tawi la Mbozi ambao walikuwa wakitokea tunduma kuelekea Vwawa.

Amesema katika ajali hiyo dereva wa Lori ambaye bado hajatambuliwa jina alibanwa mguu wa kushoto na anaendelea na matibabu hospitalini hapo na miili ya marehemu bado haijafahamika na imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti hospitalini hapo.

Mkuu wa wilaya ya Mbozi Dr Michael Kadege amesema amesikitishwa na ajali hiyo na kuwasihi madereva kuwa makini wanapokuwa barabarani kwani ajali nyingi zinasababishwa na uzembe wa madereva.

0 Responses to “AJALI MBAYA YAUA DEREVA WA NSSF NA MENEJA WAKE MBEYA”

Post a Comment

More to Read