Friday, November 7, 2014
TIKETI ZA ELEKTRONIKI KUTOUZWA KWENYE MAGARI.
Do you like this story?
Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa
wa Tanzania Bara inaendelea wikiendi hii ambapo tiketi za elektroniki
hazitauzwa tena kwenye magari, hivyo washabiki wanunue tiketi hizo kwenye
mtandao au kwenye maduka ya CRDB Fahari Huduma.
Kesho (Novemba 8 mwaka huu) kwenye Uwanja
wa Taifa, Dar es Salaam kutakuwa na mechi kati ya Yanga na Mgambo Shooting
wakati Uwanja wa Chamazi kutakuwa na mechi kati ya Azam na Coastal Union.
Jumapili ni mechi kati ya Simba na Ruvu Shooting.
Viingilio kwenye mechi za Uwanja wa Taifa
ni sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya kijani na bluu, sh. 8,000 (viti vya rangi ya
chungwa), sh. 15,000 (VIP B na C) wakati VIP A itakuwa sh. 20,000. Mechi za
Uwanja wa Chamazi kiingilio ni sh. 3,000 kwa sh. 10,000.
Mechi nyingine za VPL kesho ni kati ya
Stand United na Mbeya City (Uwanja wa Kambarage, Shinyanga), Mtibwa Sugar na
Kagera Sugar (Uwanja wa Manungu, Morogoro).
Raundi hiyo ya saba itakamilika Jumapili
kwenye Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam kwa mechi kati ya JKT Ruvu na Ndanda
kutoka Mtwara.
Wakati huo huo, mchezaji bora wa VPL kwa
mwezi Oktoba, Salum Abubakar wa Azam atakabidhiwa zawadi yake kesho (Novemba 8
mwaka huu) kabla ya mechi kati ya Azam na Coastal Union.
IMETOLEWA
NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “TIKETI ZA ELEKTRONIKI KUTOUZWA KWENYE MAGARI.”
Post a Comment