Friday, November 7, 2014
UPDATE: WATU 37 WAJERUHIWA BAADA YA BASI LA KAMPUNI YA HAPPY NATION KUPASUKA TAIRI NA KUPINDUKA
Do you like this story?
Watu37
wamejeruhiwa mara baada ya basi walilokuwa wakisafiria kutoka
mkoani Mbeya kwenda Dar es salaam kupasuka tairi na kupinduka katika eneo la
Meta, Chimala, Mbarali mbeya.
Ajali hiyo
imehusisha basi la kampuni ya Happy Nation lenye namba za usajili
T. 281 ARR Scania lililokuwa likendeshwa na dereva aliyefamika kwa jina moja la
Shabani.
Taarifa
iliyothibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya, Ahmed Msangi inasema kuwa
basi hilo lilikuwa likitokea mkoani Mbeya kuelekea mkoani Dar es Salaam.
Amesema
ajali hiyo imetokea leo Nov 7 majira ya asubuhi baada ya kupasuka
tairi la mbele kushoto hali ambayo ilisababisha kuacha njia na
kupinduka.
Amesema mara
baada ya kupasuka tairi dereva alishindwa kuimudu nahasa kutokana na eneo
lenyewe kuwa na kona kali hivyo aliamua kuligongesha kwenye ukingo wa barabara
nakusabisha hali hiyo.
Aidha Msangi amesema kuwa kati ya
majeruhi hao 29 ni wanaume na wengine 8
nakwamba hakuna mtu aliyepoteza maisha katika ajali hiyo.
Amesema kuwa
majuruhi Sita kati ya wote hali zao ni mbaya na tayari wamefikishwa
katika hospitali ya rufaa Mbeya kwa matibabu zaidi wakati majeruhi wengine 10
wakiwa wanapatiwa matibabu katika kituo cha afya Chimala.
Akithibitisha
kupokea kkwa majeruhi hao Muuguzi katika chumba cha msaada wa haraka hospitali
ya Rufaa Mbeya Dkt Orivia Masoi amesema kuwa wamepokea majeruhi sita
ambapo wanne wamelazwa wodini na wawili tayari wameruhusiwa.
Aidha mmoja wa
majeruhi Nicolaus Fungo ambaye amelelazwa wodi namba moja kwa ajili
ya matibu hao amesema majeraha makubwa maeneo ya mbavuni na kwamba hali yake
inaendelea vizuri mara baada ya kuaptiwa matibabu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “UPDATE: WATU 37 WAJERUHIWA BAADA YA BASI LA KAMPUNI YA HAPPY NATION KUPASUKA TAIRI NA KUPINDUKA ”
Post a Comment