Thursday, November 20, 2014
GHARAMA ZA KITAMBI NI SAWA NA ZA UVUTAJI
Do you like this story?
Gharama za unene wa kupitiliza duniani ni karibu sawa na
utumiaji wa bidhaa za tumbaku ukiwemo uvutaji wa sigara au sawa na gharama za
vita na kubwa kuliko unywaji wa pombe au mabadiliko ya tabia nchi, unasema
utafiti.
Taasisi ya The McKinsey Global Institute imesema inagharimu
pauni za Uingereza trilioni £1.3, au asilimia 2.8% ya shughuli ya kiuchumi kwa
mwaka - inagharimu pauni za Uingereza bilioni £47.
Watu wapatao bilioni 2.1 - kiasi cha asilimia 30% ya idadi
ya watu duniani- wana uzito wa kupita kiasi au wana vitambi, watafiti hao
wamesema.
Wamesema hatua ambazo ni wajibu wa mtu binafsi, zinatakiwa
kutumiwa ili kutatua tatizo hili.
Mtu mwenye kitambi akipima tumbo lake
Ripoti hiyo inasema kuna "gharama kubwa za
kiuchumi", na uwiano unaweza kukua kufikia karibu nusu ya idadi ya watu
duniani ifikapo mwaka 2030.
Gharama ya fedha kwa wenye vitambi inazidi kuongezeka- kwa
huduma za afya na kwa upana zaidi katika uchumi. Kwa kusababisha maradhi,
kitambi kina madhara katika utendaji wa kazi na kupotea kwa tija.
Watafiti wanasema kuwa sera zenye mwelekeo zinahitajika
kufikiriwa.
Dr Alison Tedstone, mkuu wa masuala ya lishe katika Public
Health England (PHE), amesema: "Ripoti hiyo ni mchango mzuri katika
mjadala wa vitambi. PHE imesema ujumbe wa elimu pekee haisaidii kutatua tatizo
la unene wa kupitiliza."
Dr Tedstone amesema unene wa kupita kiasi unataka hatua za
kitaifa na serikali za mitaa, viwanda na jamii kwa ujumla, na hakuna jibu moja
katika kukabiliana na hali hiyo".
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “GHARAMA ZA KITAMBI NI SAWA NA ZA UVUTAJI”
Post a Comment