Thursday, November 20, 2014
SERIKALI YATANGAZA KUJENGA BARABARA ZA KULIPIA
Do you like this story?
Serikali imetangaza
rasmi kuanza mpango wa kutengeneza barabara zitakazotumiwa kwa kulipia kutoka
Dar es salaam hadi Mkoani Morogoro.
Hatua hiyo ya
Serikali imekuja wakati foleni za barabarani zikizidi kuongezeka kwa kasi
katika jiji la Dar es salam jambo ambalo limekua likilalamikiwa na wananchi.
Waziri wa Ujenzi John
Magufuli alisema mradi huo utakua wa awamu mbili ambapo ya kwanza itaanza Dar
hadi Chalinze na nyingine Chalinze hadi Morogoro.
Alisema sababu ya
kuchukua uamuzi huo ambao umekua ukitumiwa na nchi nyingine zilizoendelea
duniani imechangiwa na tathmini iliyotolewa ikionyesha kwa siku zinapita
gari 56,000 katika barabara ya Morogoro.
“Kwa hali hii takwimu
zinaonyesha kati ya mwaka 2015 hadi2016 magari yatakuwa yakishikana
kutokana na msongamano,ndipo tukafikiria utaratibu huu ambao utasaidia watu
mbalimbali wenye uwezo wa kulipia ili wasikae katika foleni,”alisema Magufuli.
Alisema faida
zitokanazo na utumiaji wa njia hizo utasaidia kuokoa muda na kupunguza ajali
barabarani na gharama kidogo za mafuta kutokana na kuwa na mwendo kasi wa
kilomita 120 kwa saa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “SERIKALI YATANGAZA KUJENGA BARABARA ZA KULIPIA ”
Post a Comment