Thursday, November 20, 2014
MAJANGA HAYA: MENO YA TEMBO YAPOTEA MIKONONI MWA SERIKALI
Do you like this story?
Kuhusu vita dhidi ya
biashara haramu ya meno ya tembo, mataifa mbalimbali yamekuwa yakikemea
biashara hiyo lakini bado wapo watu ambao wameendelea kuifanya.
Maafisa Wanyamapori
watano wamesimamishwa kazi ili kupisha upelelezi kufanyika kufuatia kupotea kwa
meno ya tembo kwenye mazingira ya kutatanisha yakiwa katika sehemu ya ulinzi
mkali wa Serikali, Uganda.
Akizungumza na AFP
mkurugenzi wa Uganda Wildlife Authority, Raymond Engena amesema wameomba msaada
wa Kikosi cha Askari wa Kimataifa (Interpol) kufanya upelelezi kufuatia agizo
la Rais
Museveni la kutaka wahusika
wote kukamatwa kutokana na upotevu huo.
Meno hayo yana uzito
wa kilo 1,335 yana thamani ya Dola Mil. 1.1 za Uganda ambapo imesemekana baadhi
ya maofisa hao wamekuwa wakiyachukua meno hayo kwa ajili ya kutumia kuwatega
wafanyabiashara wa meno hayo lakini hawayarudishi baada ya kuyafanyia kazi
hiyo.
Ripoti zinaonyesha idadi ya tembo
35,000 wamekuwa wakiuawa Afrika kila mwaka kutokana na biashara hiyo kuonekana
kuwa na soko kubwa nchi za Asia.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ MAJANGA HAYA: MENO YA TEMBO YAPOTEA MIKONONI MWA SERIKALI”
Post a Comment