Wazazi wengi Afrika
wamekuwa hawajali kuvitambua vipaji vya watoto wao kipindi wanapokua kwenye
hatua ya utoto na wanapoanza kukua, mfano mzuri ni kwamba ukiongea na watu
ambao wana vipaji na uwezo mkubwa kwenye mchezo kama mpira wa miguu, ama kuimba
na vinginevyo utagundua kwamba jitihada binafsi zimewaongoza kugundua vipaji
vyao na mchango wa wazazi ni mdogo ama usiwepo kabisa.
Hot news kutoka
Coventry, Uingereza inamhusu Ayan Qureshi ambaye ana umri
wa miaka sita tu, na mwaka jana aliingia kwenye list ya watoto waliofanya
maajabu ambapo alifanya mtihani wa kampuni ya Microsoft unaothibitisha
wataalamu wa IT duniani na kufaulu, baba yake ambaye ni mtaalamu wa IT anasema
alimfundisha mtoto wake kuhusu masuala ya Kompyuta tangu akiwa ana umri wa
miaka mitatu.
Katika mahojiano na
mtoto huyo amesema mtihani ulikuwa mgumu lakini alienjoy kuufanya na alijiandaa
kwa miezi mingi kabla ya kuufanya, kutokana na kufaulu mtihani huo kwa sasa
anakuwa ni mtaalamu wa IT aliyethibitishwa na Microsoft ambaye ana umri mdogo
zaidi duniani.
0 Responses to “ KUTANA NA MTAALAM WA IT(Computer) MWENYE UMRI MDOGO KULIKO WOTE DUNIANI ”
Post a Comment