Wednesday, November 19, 2014
FAMILIA YA BOB MARLEY KUUZA BIDHAA ZA BANGI
Do you like this story?
Familia ya aliyekuwa mwanamuziki wa Jamaica, Bob Marley imezindua kampuni
ambayo wanaitaja kama ya kwanza duniani kuuza bidhaa za Canbbisa au marujuana
au Bangi kama wanavyoijua wengi.
Bidhaa hizo
zitajulikama kama 'Marley Natural' na na zitajumuisha mafuta ya urembo pamoja
na manukato mengine ya wanawake na bidhaa nyinginezo.
Bidhaa
hizo zitatengezwa na kampuni kubwa ijulikanano Privateer Holdings iliyo mjini
Washington Marekani, ikisisitiza kutaka kudumisha kumbukumbu ya mwanamuziki
huyo aliyesifika kote duniani.
Bidhaa
hizo zitauzwa nchini Marekani na kwingineko duniani kunzia mwaka jana.
Mwanawe
Bob Marley, Cedella Marley, alisema hayati babake angekuwa hai angefurahishwa
sana na wazo hilo.
''Babangu
angekuwa na fahari kubwa kuona watu wakitambua uwezo wa kuponya wa Bangi,''
alisema Cedella.
Mkuu wa
kampuni hiyo, Brendan Kennedy alisema Marley alikuwa mtu ambaye kwa njia nyingi
alisaidia kuanzisha harakati za kupinga juhudi za kuharamisha Bangi miaka 50
iliyopita.
"Marley
alipenda sana kutumia Bangi na hakuna aliyemshinda kwa hilo duniani kote. ''
Bob Marley
alifariki mwezi Mei mwaka 1981, kutokana na Saratani.Alipenda sana kutumia
Bangi kama sehemu ya imani yake ya Rastafarian na kuunga mkono kuhalalishwa
kwake.
Matumizi
ya Bangi kwa ajili ya kujiburudisha yamehalalishwa katika majimbo ya Colorado
na Washington nchini Marekani.
Majimbo
mengine huenda yakaidhinisha matumizi ya Bangi nchini Marekani na mengine
tayari yanaruhusu utumiaji wa bidhaa hiyo kwa sababu za matibabu.cHANZO BBC
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “FAMILIA YA BOB MARLEY KUUZA BIDHAA ZA BANGI”
Post a Comment