Wednesday, November 19, 2014
MBEYA CITY:DEUSI KASEKE BADO NI MALI YETU
Do you like this story?
Na
Emanuel Madafa, Mbeya.
KLABU ya timu ya Mbeya
City, imesema bado inamshikilia mchezaji wao Deus Kaseke na kukanusha
madai ya kwamba mchezaji huyo anatarajiwa kusajiriwa na timu za Simba na Yanga
kupitia dirisha dogo.
Kiungo huyo mshambuliaji wa
kikosi hicho cha Mbeya City, hivi karibuni jina lake limeoneka kuchomoza kwenye
vyombo vya habari ikionyesha kwamba mchezaji huyo anakwenda kwa wekundu wa
msimbazi Simba sanjari na mshambuliaji wa Mtibwa Sugar Ame Ali.
Aidha taarifa hizo zimekuwa
zikidai kuwa mchezaji huyo huenda akamwaga wino katika klabu ya Yanga kwa ajili
ya kukipiga katika duru la pili .
Akizungumza na blog
hii, Katibu mkuu wa klabu hiyo, Emmanuel Kimbe, alisema mpaka sasa
uongozi huo haujapata ofa yoyote kutoka kwenye vilabu hivyo.
Amesema, hivyo
mchezaji Deus Kaseke anaendelea kuwa mchezaji halali wa klabu ya Mbeya City
lakini Kimbe, hakuwa tayari kuweka wazi mkataba walioingia na mchezaji huyo.
Katibu huyo ameweka wazi
kuwa Mpaka sasa bado klabu hiyo inauhalali wa kuendelea kumtumia mchezaji
Deus Kaseke kwani mkataba wake haujamalizika na pia uongozi haujapokea ofa
yoyote kutoka klabu za Yanga na Simba.
Wakati huo huo, timu ya
mbeya city inatarajia kuingia kambini mwishoni mwa mwezi huu kujiwinda na duru
inayofuata ya ligi kuu ya soka ya Tanzania Bara.
Timu hiyo ambayo itafungua
dimba na timu ya Ndanda kutokaa Mkoani Mtwara, mchezo unaotaraji kupigwa kwenye
dimba la kumbukumbu ya hayati Edward Moringe Sokoine Jijini Mbeya.
Hata hivyo, msimu huu timu
hiyo haijafanikiwa kufanya vizuri baada ya kufungwa michezo minne kwenda sare
michezo mitatu na kupata ushindi wa mchezo mmoja dhidi ya Costunion ya Tanga
hivyo kujikusanyia jumla ya pointi 5 ikiwa inaburuza mkia kwenye msimamo wa
ligi kuu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MBEYA CITY:DEUSI KASEKE BADO NI MALI YETU”
Post a Comment