Wednesday, November 19, 2014
WAPINZANI WAMSULUBU MWAKYEMBE.
Do you like this story?
Dodoma. Kambi Rasmi
ya Upinzani Bungeni, jana ilimsulubu Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe
ikieleza kuwa wizara yake iliingia mkataba wa mradi wa treni za kisasa kutoka
Stesheni ya Dar es Salaam hadi Pugu kupitia Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere
(JNIA) bila kufuata taratibu.
Kambi hiyo ililieleza Bunge kuwa mkataba huo
ulisainiwa baina ya mmiliki wa Kampuni ya M/s Shumoja, Robert Shumake na
Shirika la Reli Tanzania huku Waziri Mwakyembe akishuhudia.
Gekul alisema taratibu hazikufuatwa kwa kuwa
haieleweki ni lini Serikali, wakala au Wizara ya Uchukuzi ilitangaza zabuni ya
mradi wa treni kutoka Stesheni hadi Pugu kupitia JNIA.
“Pia haijulikani ni lini Serikali ilifanya upembuzi
yakinifu kuhusu mradi huo wa reli kwa kufuata taratibu kama zinavyoainishwa na
Sheria ya PPP ya mwaka 2010 ambayo inafanyiwa marekebisho hivi sasa,” alisema
Gekul na kuongeza: “Haijulikani ni kampuni ngapi ambazo ziliomba tenda ya
ukandarasi wa treni na kwamba M/s Shumoja ilishinda tenda hiyo kwa vigezo
gani.”
Alisema kwa kifupi ni wazi kuwa Dk Mwakyembe na wizara
yake walikiuka vifungu vya Sheria ya PPP. Alivitaja vifungu hivyo kuwa ni 4(1)
na (2) vinavyomtaka waziri kutangaza katika Gazeti la Serikali miradi
mbalimbali inayotegemewa kufanywa na sekta ya umma kwa ubia na sekta binafsi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “WAPINZANI WAMSULUBU MWAKYEMBE.”
Post a Comment