Thursday, March 10, 2016
NDALICHAKO: VYETI VYA FORM SIX VILIVYO KATIKA MFUMO WA GPA HAVITABADILISHWA KWENDA DIVISION
Do you like this story?
Serikali
imesema haina mpango wa kubadili vyeti vya wanafunzi waliomaliza kidato cha
sita mwaka jana kutoka kwenye mfumo wa alama za GPA kwenda Divisheni.
Msimamo huo wa
serikali, umetolewa na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya
Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako.
Amesema
serikali haina mpango wa kubadili mfumo huo wa vyeti kwani tangu awali
wanafunzi walisoma kwa mfumo wa GPA na vyeti vilitoka kwa mfumo huo.
“Hatuwezi
kubadili vyeti hivyo, isipokuwa vimehitajika kwa ajili ya marekebisho madogo
ambayo Katibu Mkuu wa Wizara, aliyasema lakini siyo kubadili kwenda mfumo wa
divisheni,” alisema.
Februari mwaka
huu, Baraza la Taifa la Mitihani (Necta), lilitangaza kusitishwa kwa ugawaji wa
vyeti vya kidato cha sita kwa wanafunzi waliohitimu mwaka 2015, huku likiagiza
kuwa vile vilivyokwisha gawanywa kwa wahitimu hao vinatakiwa kurejeshwa kwenye
chombo hicho.
Hata hivyo,
Katibu Mtendaji wa Necta, Dk, Charles Msonde, hakubainisha marekebisho ambayo
wanatakiwa kuyafanya kwenye vyeti hivyo na badala yake kudai baraza linataka
kujiridhisha na baadhi ya vitu.
Hatua hiyo ya
kubadili vyeti hivyo iliibua utata mkubwa, huku baadhi ya wadau wakiwamo maofisa
elimu, wakihisi Necta huenda inalenga kuvibadili vyeti hivyo kutoka kwenye
mfumo wa wastani wa alama (GPA), kwenda kwenye ule wa jumla (division).
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ NDALICHAKO: VYETI VYA FORM SIX VILIVYO KATIKA MFUMO WA GPA HAVITABADILISHWA KWENDA DIVISION”
Post a Comment