Thursday, March 10, 2016
ATUPWA JELA MIAKA 7 KWA KUMKATA MKEWE SEHEMU ZA SIRI ILI APATE MALI.
Do you like this story?
Mkazi wa Kata
ya Mbugani, Manispaa ya Tabora, Mashaka Maziku (60) amehukumiwa kifungo cha
miaka saba jela kwa kosa la kumkata sehemu za siri mkewe kwa imani za
kishirikina ili apate mali.
Hakimu Joctan
Rushwela alisema jana kuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Tabora imeridhishwa
na ushahidi uliotolewa upande wa mashtaka.
Hakimu Rushwela
alisema anamhukumu mshtakiwa huyo kwenda jela ili iwe fundisho kwa wengine
wanaokuwa na tamaa ya kujipatia mali kwa njia za kishirikina.
Awali wakili wa
Serikali, Idd Mgeni alidai kuwa mshtakiwa huyo na mganga wa jadi, walitenda
kosa hilo kati ya Oktoba 29 na Novemba 2, 2014 katika eneo la Kazaroho Kata ya
Mbugani, Manispaa ya Tabora.
Wakati wa tukio
hilo, ilidaiwa kuwa Maziku aliambiwa na mganga huyo ambaye ni mshtakiwa wa pili
katika kesi hiyo, Kahele Paul kwamba akipeleka sehemu za siri za mkewe atapata
Sh5milioni.
Alidai baada ya
kupewa ushauri huo, alimchukua mkewe na kwenda kumnywesha pombe ili aweze
kutimiza ukatili huo.
Alidai baada ya
kunywa pombe nyingi, alichukua kisu na kumkata sehemu za siri mkewe na
kuzihifadhi kwenye mfuko wa suruali yake na kutoweka.
Alidai kwa
mujibu wa mashahidi wanne, mwanamke huyo alikuwa akipiga kelele kutokana na
maumivu makali aliyopata huku akivuja damu nyingi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ ATUPWA JELA MIAKA 7 KWA KUMKATA MKEWE SEHEMU ZA SIRI ILI APATE MALI.”
Post a Comment