Thursday, September 15, 2016
HATUA ZILIZOCHUKULIWA NA KWA VIJANA 5 WALIOMDHALILISHA RAIS MAGUFULI NA JESHI LA POLISI TANZANIA
Do you like this story?
Vijana watano wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kumdhalilisha
Rais Dk. John Magufuli na Jeshi la Polisi kutokana na mauaji ya askari polisi
wanne waliouawa na majambazi katika eneo la Mbande na Vikindu, Dar es Salaam
hivi karibuni.
Washitakiwa hao walifikishwa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu, Dar es Salaam mbele ya mahakimu watano tofauti na kusomewa mashtaka na
Wakili wa Serikali, Salum Mohammed.
Walisomewa mashitaka mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Emmilius Mchauru,
Huruma Shahidi, Margareth Bankika, Dk. Yohana Yongolo na Respicius Mwijage.
Akisomewa mashtaka, mshtakiwa Dennis Mtegwa anadaiwa Agosti 24,
mwaka huu eneo la Ubungo External kupitia mtandao wa WhatsApp, aliweka
maoni katika group linaloitwa Dsm 11 4u Movement, akisema ‘JPM sijui anawaza nini kichwani… hata
samahani hajui au nilikosea hajui’, ‘nchi imefika hapa kwa sababu ya mtu
mmoja aliyeamua kujilipua ufahamu wake’, ‘sijaona tatizo kwa hilo, ila kwa huyu
bwana misimamo ambaye amesema msinijaribu na ilhali kajaribiwa na ubwabwa wa
jubilee kusema yote’.
‘Siasa si chuki wala upinzani si
uadui, ajifunze kushindana kwa hoja sio mitutu ya bunduki na mazoezi yasiyo na
kichwa wala miguu ya polisi’.
Mshtakiwa Suleiman Saidi anadaiwa Agosti 25, mwaka huu maeneo ya
Kigogo, kwa kutumia mtandao wa Facebook, aliandika ‘Safi sana aisee, mi naona wangekufa kama 20
hivi halafu Simon Sirro tumuulize mazoezi wanafanyia wake zao au’.
Katika kesi nyingine, mshtakiwa Juma Mtatuu akiwa eneo la Ocean
Road, Agosti 24, mwaka huu anadaiwa kuwa alituma ujumbe katika Facebook akisema ‘Huyu hata akifa ataenda peponi, na kufanya
mazoezi kote kule wamekufa Mbagala, mimi nitakuwa wa kwanza kuandamana
kule Kahama, tarehe moja naelekea Kahama kwa Ukuta, mimi nitakuwa namba
moja kushika bendera ya Ukuta, kifo kipo tuu, usiogope kwani mawe na mapanga
yameisha’
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


.gif)


0 Responses to “ HATUA ZILIZOCHUKULIWA NA KWA VIJANA 5 WALIOMDHALILISHA RAIS MAGUFULI NA JESHI LA POLISI TANZANIA”
Post a Comment