Thursday, September 15, 2016
KIWANDA CHA TANZANIA CHAONGOZA KWA UBORA BARANI AFRIKA
Do you like this story?
![]() |
| Wafanyakazi wa TBL Mbeya wakiwa nje ya lango kuu la kuingilia ofisini kwao. |
![]() |
| Wafanyakazi wa kiwanda cha Bia cha TBL- Mbeya, wakionyesha kombe na cheti cha ushindi mitaani wakati wa mapokezi ya Meneja wa Kiwanda hicho. |
Wakati serikali ya
awamu ya tano inajipanga kuifanya Tanzania nchi ya viwanda tayari dalili njema
zimeishajitokeza kuwa watanzania tukiamua tunaweza kwa kuwa kiwanda
kinachoshikilia rekodi ya ubora barani Afrika ni kiwanda cha kutengeneza Bia
cha TBL kilichopo katika kitongoji cha Iyunga mkoani Mbeya.
Kwa mara nyingine
tena baada ya kushindanishwa na viwanda vikubwa vipatavyo 21 barani
Afrika,mwishoni mwa wiki iliyopita TBL Mbeya imeibuka kinara na kutangazwa kuwa
kiwanda bora barani Afrika kati ya viwanda vilivyopo chini ya kampuni kubwa
yenye viwanda vya kutengeneza bia duniani ya SABMiller na kimelinda rekodi yake
kilichokuwa kinaishikilia.
Rekodi hii inaenda
sambamba na dhamira ya serikali ya kuifanya Tanzania nchi ya viwanda na
inadhihirisha kuwa uwekezaji wa viwanda sio lazima ufanywe maeneo ya mijini
kama ambavyo ilikuwa imezoeleka kwa muda mrefu.
Mhandisi Jemedari
Waziri,Meneja wa kiwanda hiki akiongelea mafanikio haya alisema kuwa anajivunia
ushindi huu kwa kuwa ni uthibitisho halisi kuwa watanzania tunaweza kufanya
vizuri na kuleta maendeleo kwa kasi tukiamua.
“Tunaposema ubora wa
kiwanda tunaamaanisha ubora wa bidhaa tunazozalisha,teknolojia tunazotumia,raslimali
watu tuliyonayo,mchango wa kiwanda kwa serikali na jamii iliyotuzunguka bila
kusahau utunzaji wa mazingira ambayo ni moja ya nguzo ya kampuni yetu”.Alisema.
Aliongeza kuwa
ushindi huu ni kwa wana Mbeya wote na wana kanda ya Nyanda za Juu Kusini
“Tunawashukuru wateja wetu wote kwa kutuunga mkono wakati wote na tutaendelea
kuwaletea bidhaa bora kwenye soko na kubuni miradi mbalimbali ya kijamii
itakayosaidia kuleta mabadiliko”.Alisema
Jemedari pia alisema
ushindi huu unatokana na jitihada za pamoja kutoka kwa wafanyakazi wote wa
kiwanda na TBL Group kwa jumla na anafurahi kuona kiwanda kinaendeshwa na
watanzania asilimia kubwa ikiwa ni vijana wenye vipaji vya ajabu na waliobobea
katika fani mbalimbali.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


.gif)




0 Responses to “ KIWANDA CHA TANZANIA CHAONGOZA KWA UBORA BARANI AFRIKA”
Post a Comment