Thursday, September 15, 2016
JK ATOA YA MOYONI KUHUSU RAIS MAGUFULI KUTOKWENDA ZAMBIA
Do you like this story?
Rais
mstaafu, Jakaya Kikwete ameunga mkono uamuzi wa Rais John Magufuli kuahirisha
safari kwenda nje ya nchi ili kushiriki katika maafa ya tetemeko la ardhi
lililotokea mkoani Kagera.
Kikwete
amesema uamuzi huo ni wa busara kwa kuwa Serikali inatakiwa kufanya juhudi za
makusudi kushughulikia tatizo hilo.
Kikwete
aliyemtumia salamu za pole Dk Magufuli na waathirika wa tukio hilo, amesema
misaada ya haraka na dharura inahitajika ili waathirika waendelee kupata huduma
zote muhimu hasa za kibinadamu.
Kiongozi
huyo mstaafu ameyasema hayo katika hafla ya makabidhiano ya nyumba 22 za
watumishi wa afya, 10 zikiwa Chalinze, mbili Bagamoyo na nyingine 10 Mafia
zilizojengwa na Taasisi ya Benjamin Mkapa mkoani Pwani.
“Ndugu
zangu pamoja na leo hii tunakabidhiana nyumba 22 za watumishi wa afya mkoani
kwetu, naomba tusimame tuwakumbuke wenzetu waliopoteza maisha katika tetemeko
la ardhi huko Bukoba na pia natumia fursa hii kutoa pole kwa waathirika wote na
Rais Dk Magufuli,” amesema.
Ameongeza
kuwa: “kiukweli amefanya uamuzi wa busara kuahirisha safari yake ili
kushiriki katika maafa haya.”
Hafla
ya makabidhiano hayo imefanyika katika Kituo cha Afya Msoga, Chalinze.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


.gif)


0 Responses to “ JK ATOA YA MOYONI KUHUSU RAIS MAGUFULI KUTOKWENDA ZAMBIA”
Post a Comment