Saturday, March 12, 2016
WAVAA "VIMINI" WAVULIWA NGUO HADHARANI JIJINI MBEYA.
Do you like this story?
Wasichana wanaovaa nguo fupi za kubana na wavulana wanaovaa
milegezo jijini Mbeya , juzi walipata wakati mgumu baada kundi la vijana
kuwavua nguo zao na kuzichana hadharani, kutokana na gari la matangazo kupita
jijini hapa likiwataka watu kuvaa nguo za heshima zinazoendana na maeneo
husika.
Tangu Machi 7 hadi 9, gari la matangazo ya Kampuni ya Studio
H ya Huruma lilipita mitaa mbalimbali ya jijini Mbeya, likiwataka wasichana
kuacha kuvaa vimini na vijana kuacha kuvaa mlegezo.
Baada ya tangazo hilo, vijana walianza kuwavamia wasichana
na wavulana waliovaa milegezo maeneo ya Uyole, Soweto, Kabwe na Mwanjelwa, huku
wanawake waliokuwa wakiuza matunda wakiwarushia vitenge wasichana waliochaniwa
nguo ili wajisitiri.
Ofisa Habari Jiji la Mbeya, John Kilua alisema uongozi
hauhusiki na tangazo hilo.
Hata hivyo, Ofisa wa Kampuni ya Studio H ya Huruma, Siyata
Mbua alisema walitoa tangazo hilo baada ya kukamilika kwa makubaliano baina ya
jiji na kampuni yake.
Mbua alisema kazi ya kuzuia nguo zisizo za heshma inahusu
Serikali, lakini kampuni iliamua kujitolea kwa makubaliano na jiji kwa mwaka
mmoja.
“Lengo ni kuwahamasisha wananchi wavae nguzo za heshima.
Hatuwahamasishi vijana wawavamie watu, bali tunawataka kila mmoja avae nguo
kulingana na maeneo anayofanyia kazi,”alisema.
Mabua alisema lengo ni kuelimishana zaidi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi alisema
hajapata malalamiko na kuwataka vijana kuheshimu utu wao kwa kuvaa nguo za
heshima.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “WAVAA "VIMINI" WAVULIWA NGUO HADHARANI JIJINI MBEYA.”
Post a Comment