Wednesday, February 3, 2016

YANGA YATULIZWA NA ‘WAJELAJELA’ MBEYA


Mashabiki wa Tanzania Prisons wakishangilia mara Baada ya kupata Goli la Pili(Picha na David Nyembe wa Fahari News)







(Picha na David Nyembe wa Fahari News)


Baada ya ya Yanga kuchezea kibano weekend iliyopita, leo wameambulia sare mbele ya Tanzania Prisons ‘Wajelajela’ wa mkoani Mbeya kwa kufungana magoli 2-2 kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara uliochezwa kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Yanga walikuwa wakwanza kupata goli la kuongoza kupitia kwa Amis Tambwe dakika ya 35 akiunganisha krosi iliyopgwa na Haruna Niyonzima lakini bao hilo lilisawazishwa na Jeremia Juma Mgunda dakika ya 40 akimalizia krosi ya Mohamed Mkopi.

Mohamed Mkopi aliiandikia Prisons bao loa pili dakika ya 62 kipindi cha pili akiunganisha kwa kichwa mpira wa adhabu ndogo uliopigwa na kiungo wa zamani wa Yanga Juma Seif Kijiko.

Simon Msuva aliiokoa Yanga kwenye janga la kuchezea kichapo baada ya kuisawazishia Yanga kwa mkwaju wa penati baada ya beki wa Prisons Meshack Suleimani kuunawa mpira kwenye eneo la hatari kisha mwamuzi kuamuru upigwe mkwaju wa penati ambao ulikwamishwa wavuni ya Simon Msuva.

Yanga bado wanaendelea kuongoza ligi wakiwa na pointi 40 wakiwa wameshacheza mechi 17 wakifatiwa na Azam FC wenye pointi 39 sawa na Simba lakini Azam wao wanafaida ya michezo miwili mkononi wakiwa hawajacheza mechi hizo kutokana na kushiriki mashindano ya kirafiki nchini Zambia ambako wamealikwa.

0 Responses to “YANGA YATULIZWA NA ‘WAJELAJELA’ MBEYA”

Post a Comment

More to Read