Wednesday, February 3, 2016

SIMBA SASA MGONGONI KWA YANGA






Simba imeendelea kuthibitisha inautaka ubingwa wa ligi ya Vodacom msimu huu baada ya leo kufanikiwa kuchomoza na ushindi wa bao 5-1 dhidi ya Mgambo JKT ikiwa ni ushindi wa nne mfululizo kwa Mayanja kwenye mechi za ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara baada ya kujiunga na Simba kama kocha msaidizi akitokea Coastal Union.

Mabao ya Simba yamefungwa na Hamisi Kiiza ambaye ametupia bao mbili wavuni na sasa amemfikia Amis Tambwe wa Yanga kwa kufikisha bao 14 na kinyang’anyiro cha mfungaji bora kuwa kitamu zaidi.

Magoli mengine ya mnyama yamekwamishwa kambani na Daniel Lyanga, Ibrahim Ajib na Mwinyi Kazimoto ambao wote wamefunga bao moja moja.

Ushindi huo unarejesha matumaini makubwa kwa Simba ya kunyakua ubingwa kwasababu imefikisha pointi 39 sawa na Azam ambayo ipo nafasi ya pili licha ya Simba kuwa mbele ya Azam kwa michezo miwili lakini patamu ni pale Simba ambapo inatofautiana kwa pointi moja na watani wao wa jadi Yanga ambao leo wamebanwa mbavu na kulazimisha sare dakika za lala salama dhidi ya Tanzania Prisons.

Yanga bado inaongoza ligi kwa pointi 40 ikifuatiwa na Azam yenye pointi 39 sawa na Simba ambayon ipo nafasi ya tatu lakini ikitofautiana na Azam kwa magoli ya kufunga na kufungwa  japo Simba wanaizidi Azam kwa michezo miwili.

Matokeo ya mechi zote zilizochezwa leo yapo hapo chini:
Mtibwa Sugar 2-2 Toto Africans
African Sports 1-0 Mwadui FC
Kagera Sugar 2-1 Majimaji
Simba SC 5-1 Mgambo JKT
Tanzania Prisons 2-2 Yanga

0 Responses to “SIMBA SASA MGONGONI KWA YANGA”

Post a Comment

More to Read