Thursday, February 4, 2016
MAKUMBUSHO YA KWANZA KUWA CHINI YA MAJI, SASA WATEMBELEAJI WATATAKIWA KUOGELEA KUSHUHUDIA MAAJABU YAKE
Do you like this story?
Jason deCaires Taylor akiwa chini ya maji kwenye masanamu aliyotengeneza. |
Masanamu hayo yanavyoonekana chini ya maji. |
Tayari Bara la Ulaya wameweza kufanya kitu cha ajabu zaidi baada ya
kuanzisha Makumbusho maalum ambayo ipo chini ya bahari. Kwa hatua hiyo
watembeleaji itawataka kutembelea humo kwa njia ya kuogelea na mavazi maalum
ili kushuhudia maajabu ya makumbusho hayo chini ya maji.
Kwa mujibu wa mtandao wa Kimataifa wa (CNN) umefafanua kuwa Ulaya
inakuwa bara la kwanza kuwa na makumbusho hiyo ya chini ya bahari katika kisiwa
cha Lanzarote.
Makumbusho hayo ni masanamu mbalimbali yaliyoingizwa humo huku yakiwa na kumbukumbu
ya watu maarufu waliowahi kuwapo duniani ambapo msanii wa masanamu hayo
amebainisha kuwa kuwapo baharini humo ni Ulinzi wa bahari.
Msanii wa kimataifa Jason deCaires Taylor aliyetengeneza masamu hayo
amebainisha kuwa, ametengeneza masanamu hayo kwa mazingira ya kirafiki ya
saruji huku akiamini kuwa, yataongeza uelewa wa masuala ya bahari.
Masanamu hayo yapo chini ya umbali wa mita kati ya 12 na 15 chini ya
bahari huku yakionekana kama kundi la watu (sanamu) wakitembea chini ya
mawimbi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ MAKUMBUSHO YA KWANZA KUWA CHINI YA MAJI, SASA WATEMBELEAJI WATATAKIWA KUOGELEA KUSHUHUDIA MAAJABU YAKE”
Post a Comment